803 Ni kwa Kumjua Mungu tu Ndiyo Unaweza Kumwabudu kwa Kweli

1 Hakuna wowote wanaomjua Mungu na kumwona Mungu kwa kweli ambao hawamwabudu Yeye, ambao hawamheshimu. Wote lazima wasujudu na kumwabudu Yeye. Kwa sasa, wakati wa kazi ya Mungu mwenye mwili, kadri watu wanavyokuwa na ufahamu wa tabia ya Mungu mwenye mwili na wa kile Alicho nacho na kile Alicho, ndivyo wanavyovithamini zaidi na kumcha Yeye. Kwa kawaida, ufahamu mdogo unamaanisha kutokuwa makini zaidi, na kwamba Mungu anachukuliwa kama mwanadamu. Ikiwa watu wanamjua Mungu na kumwona kweli, watatetemeka kwa hofu. Kwa nini Yohana alisema, “Yeye anayekuja baada ya mimi ni mwenye nguvu kuniliko, ambaye mimi si wa kufaa kubeba viatu vyake”? Ijapokuwa ufahamu wa ndani ya moyo wake haukuwa wa kina kirefu sana, lakini alijua kwamba Mungu ni wa ajabu.

2 Ikiwa watu hawajui kiini cha Kristo na hawaelewi tabia ya Mungu, hawawezi hata kumwabudu Mungu wa vitendo kwa kweli. Ikiwa watu wanaona tu kuonekana kwa nje kwa kawaida kwa Kristo na hawajui asili Yake, ni rahisi kwa wao kumchukulia Kristo kama mtu wa kawaida. Huenda wakachukua mtazamo usio wa heshima Kwake, wanaweza kumdanganya, kumkataa, kutomtii, na kutoa hukumu Kwake. Wanaweza kujiona kuwa sahihi na kuchukulia neno Lake kama yasiyo na maana, wahodhi mawazo kumhusu Mungu, na kumshutumu na kumkufuru. Ili kutatua masuala haya mtu lazima ajue kiini cha Kristo, uungu wa Kristo. Hiki ndicho kipengele kikuu cha kumjua Mungu; ni kile waumini wote wanaoamini katika Mungu wa utendaji wanapaswa kuingia na kufanikisha.

Umetoholewa kutoka katika “Jinsi ya Kumjua Mungu Mwenye Mwili” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 802 Ni Wale tu Wanaomjua Mungu Ndio Wanaoweza Kumpata Mungu

Inayofuata: 804 Matokeo Yanayofanikishwa na Kumjua Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

64 Upendo wa Kweli

1Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao,nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini.Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

125 Nimeuona Upendo wa Mungu

1Mwenyezi Mungu, ni Wewe unayenipenda.Katika ulimwengu mchafu Umenichagua mimi!Hivyo nimekuja mbele Yako, naam, nimekuja mbele Yako,...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki