291 Nani Awezaye Kumjua Mungu Ajapo?

1 Machoni Pangu, mwanadamu ndiye mtawala wa vitu vyote. Nimempa mamlaka si haba, Nikimwezesha kusimamia vitu vyote duniani—nyasi iliyo juu ya milima, wanyama katika misitu, na samaki majini. Badala ya kuwa na furaha kwa sababu ya haya, mwanadamu anasumbuliwa na wasiwasi. Maisha yake yote ni yale ya maumivu makali, na kukimbia hapa na pale, na raha kuongezwa kwa utupu, na katika maisha yake yote hakuna uvumbuzi na uundaji mpya. Hakuna anayeweza kujinasua kutoka katika utupu huu wa maisha, hakuna ambaye amegundua maisha ya maana, na hakuna ambaye amepitia maisha ya kweli.

2 Ingawa watu wa leo wote wanaishi chini ya mwanga Wangu unaong’aa, hawajui lolote kuhusu maisha ya mbinguni. Nisipokuwa na huruma kwa mwanadamu na Nisipomwokoa binadamu, basi watu wote wamekuja bure, maisha yao duniani hayana maana, na wataondoka bure, bila chochote cha kujigamba nacho. Watu wa kila dini, nyanja ya jamii, taifa, na dhehebu wote wanajua utupu ulio duniani, na wote wananitafuta na kungoja kurejea Kwangu—ilhali nani ana uwezo wa kunifahamu nitakapofika?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 25” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 290 Mpango wa Mungu Haujawahi Kubadilika

Inayofuata: 292 Watu Hawajui Wokovu wa Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp