91 Kazi ya Siku za Mwisho ni Hasa ili Kumpa Mwanadamu Uzima

1 Katika hatua hii ya mwisho ya kazi, matokeo yanapatikana kupitia kwa neno. Kupitia kwa neno, mwanadamu anaelewa mafumbo mengi na kazi ya Mungu katika vizazi vilivyopita; kupitia kwa neno, mwanadamu anapewa nuru na Roho Mtakatifu; kupitia kwa neno, mwanadamu anapata kuelewa mafumbo ambayo hayajawahi kuelezwa na vizazi vilivyopita, na pia kazi za manabii na, mitume wa enzi zilizopita, na kanuni ambazo walitumia kufanya kazi; kupitia kwa neno, mwanadamu anatambua tabia ya Mungu Mwenyewe, na pia uasi na pingamizi ya mwanadamu, na anakuja kujua dutu yake mwenyewe. Kupitia kwa hatua hizi za kazi na maneno yote yaliyonenwa, mwanadamu anatambua kazi ya Roho Mtakatifu, kazi ya mwili wa Mungu, na zaidi ya hayo, tabia Yake yote.

2 Maarifa yako ya kazi ya usimamizi wa Mungu wa kupita miaka elfu sita ulitwaliwa kupitia kwa neno. Je, maarifa yako hayakuwa ya fikira zako za awali na mafanikio kwa kuyaweka kando pia yalipatikana kupitia neno? Katika hatua ya awali, Yesu Alifanya ishara na maajabu, lakini sio hivyo katika hatua hii. Je si kuelewa kwako kwa nini Mungu hafanyi ishara na maajabu pia kulipatikana kupitia neno? Kwa hivyo, maneno yanenwayo katika hatua hii, yanashinda kazi iliyofanywa na mitume na manabii wa vizazi vilivyopita. Hata unabii uliotabiriwa na manabii haungeweza kupata matokeo haya. Kwa maneno yaliyonenwa katika hatua hii, kuna unabii na ukweli, lakini hasa yanafanya kazi ya kutawaza maisha juu ya mwanadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Fumbo la Kupata Mwili (4)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 90 Neno la Mungu ni Mamlaka na Hukumu

Inayofuata: 92 Katika Siku za Mwisho, Mungu Anatimiza Yote Kupitia Maneno Yake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp