691 Kuja kwa Magonjwa ni Upendo wa Mungu

1 Mwenyezi Mungu, Mkuu wa vitu vyote, hushika madaraka Yake ya kifalme kutoka kwa kiti Chake cha enzi. Yeye hutawala ulimwengu na vitu vyote na Yeye yuko katika harakati ya kutuongoza katika dunia yote. Kila wakati tutakuwa karibu na Yeye, na kuja mbele Zake kwa utulivu; kamwe hatutakosa wakati mmoja, na kuna mambo ya kujifunza wakati wote. Mazingira yanayotuzunguka pamoja na watu, mambo na vitu, yote yameruhusiwa na kiti Chake cha enzi. Usiwe na moyo wa kunung’unika, au Mungu hatatupa neema Yake juu yako.

2 Wakati ugonjwa hutokea ni kwa sababu ya upendo wa Mungu, na nia Yake nzuri kwa hakika inaiunga mkono. Hata wakati mwili wako unavumilia mateso, usichukue ushauri kutoka kwa Shetani. Sifu Mungu katikati ya ugonjwa na furahia Mungu katikati ya sifa yako. Usikate tamaa unapokabiliwa na ugonjwa, endelea kutafuta na kamwe usisalimu amri, na Mungu Ataangaza nuru Yake kwako. Ayubu alikuwa mwaminifu kiasi gani? Mwenyezi Mungu ni daktari mwenye nguvu zote! Kukaa katika ugonjwa ni kuwa mgonjwa, lakini kukaa katika roho ni kuwa mzima. Kama unayo pumzi moja tu, Mungu hatakuacha ufariki.

3 Ndani yetu tuna uzima wa Kristo Aliyefufuka. Bila shaka, hatuna imani mbele ya Mungu: Na iwe kwamba Mungu Atie imani ya kweli ndani yetu. Neno la Mungu ni tamu kweli! Neno la Mungu ni dawa yenye nguvu! Tilia aibu mapepo na Shetani! Kama sisi tutafahamu neno la Mungu tutakuwa na msaada na neno Lake litaokoa mioyo yetu kwa haraka! Linaondoa vitu vyote na kuweka yote kwa amani.

4 Imani ni kama daraja moja la gogo la mti, wale ambao hushikilia maisha kwa unyonge watakuwa na ugumu katika kulivuka, lakini wale ambao wako tayari kujitolea wenyewe wanaweza kulivuka bila wasiwasi. Kama mtu ana mawazo ya uoga na ya kuogofya, wao wanadanganywa na Shetani. Ina hofu kwamba tutavuka daraja la imani ili kuingia katika Mungu. Shetani hubuni kila njia iwezekanayo kututumia mawazo yake, tunapaswa daima kuomba kwamba nuru ya Mungu itatuangazia sisi, na ni lazima daima tumtumainie Mungu kututakasa kutoka kwa sumu ya shetani. Daima tutakuwa tukitenda katika roho zetu kuja karibu na Mungu. Tutamruhusu Mungu kuwa na utawala juu ya asili yetu yote.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 6” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 690 Lazima Utafute Mapenzi ya Mungu Ugonjwa Unapotokea

Inayofuata: 692 Mtazamo Wa Mwanadamu Kwa Majaribu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp