715 Huu ni Mfano wa Mtu halisi

1 Katika imani yako kwa Mungu, lazima usome maneno Yake zaidi kabla ya kuuelewa ukweli; ni kwa kuuelewa ukweli tu ndipo unaweza kujijua na kuweza kutambua na kuwa na wazo lililo wazi kuhusu tabia zipi potovu ulizo nazo. Kutenda ukweli na kuishi mbele za Mungu, lazima uusaliti mwili wako na uanze vita dhidi ya vitu unavyovipenda, vitu unavyovitamani, na tabia zako za kishetani. Ikiwa kwa kweli watu wanachukia kabisa tabia zao za kishetani na kwa kweli wanachukia matamanio ya mwili, basi wanaweza kutenda kwa makusudi kulingana na ukweli, na vitendo vyao vitakuwa vyenye maadili, vitakuwa na uwezo, na kuwa na mipaka; haya ni matokeo yanayopatikana kwa kuuelewa ukweli. Ikiwa hawauelewi ukweli, basi watatawaliwa na kufungwa na mwili daima, na hawatakuwa na njia ya kusonga mbele.

2 Watu wakipitia hadi siku ifike ambapo mtazamo wao wa maisha, na umuhimu na msingi wa kuwepo kwao yamebadilika kabisa, wakati wamebadilishwa kabisa, na wamekuwa mtu mwingine, je, jambo hili halitakuwa la kushangaza? Haya ni mabadiliko makubwa, mabadiliko ya kushangaza sana. Ni wakati tu ambapo hujali umaarufu na utajiri, hadhi, pesa, starehe, na anasa za dunia, na unaweza kuziacha kwa urahisi, ndipo utakuwa na mfanano wa binadamu. Wale ambao watafanywa kamili hatimaye ni kundi kama hili; wataishi kwa ajili ya ukweli, kuishi kwa ajili ya Mungu, na kuishi kwa ajili ya kile ambacho ni cha haki. Buu ndio mfanano wa binadamu wa kweli.

Umetoholewa kutoka katika “Kuelewa Visawe na Tofauti katika Asili ya Binadamu” katika Kumbukumbu za Maongezi ya Kristo

Iliyotangulia: 714 Wale Walio na Mabadiliko ya Tabia Wanaweza Kuishi Kama Binadamu

Inayofuata: 716 Ni Wale tu walio na Ukweli Wanaweza Kuishi kwa Kudhihirisha Maisha Halisi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

137 Nitampenda Mungu Milele

1Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako.Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku.Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu na...

760 Upendo Safi Bila Dosari

1Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari.Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza.Upendo hauweki masharti au...

901 Mradi tu Usimwache Mungu

Upendo na huruma za Mungu hupenyeza katika kila sehemu ya kazi ya usimamizi Wake, na bila kujali kama watu wanaweza kuelewa nia njema za...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki