545 Ishi Kulingana na Maneno ya Mungu Kubadili Tabia Yako

1 Lazima kwanza utatue matatizo yote ndani yako kwa kumtegemea Mungu. Komesha tabia zako potovu na kuwa na uwezo wa kuelewa kweli hali zako mwenyewe na kujua jinsi unapaswa kufanya mambo; endelea kushiriki chochote ambacho hukielewi. Haikubaliki kwa mtu kutojijua. Uponye ugonjwa wako mwenyewe kwanza, na kwa njia ya kula na kunywa maneno Yangu zaidi, kutafakari maneno Yangu, ishi maisha na fanya mambo kwa mujibu wa maneno Yangu; haijalishi ukiwa nyumbani au mahali pengine, unapaswa kumruhusu Mungu atwae nguvu ndani mwako. Uache mwili na uasili. Daima yaruhusu maneno ya Mungu yawe na mamlaka ndani mwako. Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kwamba maisha yako hayabadiliki; utakuja polepole kuhisi kwamba tabia yako imebadilika kiasi kikubwa.

2 La muhimu sasa ni kulenga kuhusu maisha, kula na kunywa zaidi maneno Yangu, upate uzoefu wa maneno Yangu, kuyajua maneno yangu, kuyafanya maneno yangu kwa dhati kuwa maisha yako—hili ni jambo kuu. Je, maisha ya mtu ambaye hawezi kuishi kwa kutegemea maneno ya Mungu yanaweza kukomaa? Lazima uishi kwa kutegemea maneno Yangu kila wakati. Katika maisha, lazima maneno Yangu yawe kanuni yako ya vitendo. Yatakusababisha kuhisi kuwa kufanya mambo kwa njia fulani ni kile Mungu anafurahia, na kufanya mambo kwa njia nyingine ni kile Mungu anachochukia; polepole, utakuja kutembea katika njia sahihi.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 22” ya Matamko ya Kristo Mwanzoni katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 544 Wale Wanaopenda Ukweli Watapata Ukweli

Inayofuata: 546 Mungu Huwapenda Wale Wanaofuatilia Ukweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp