Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

944 Kuishi kwa ajili ya Kutimiza Wajibu Wako Kuna Maana

1 Ni hawa wanaokubali kazi ya Mungu ya siku za mwisho ambao ni wenye akili zaidi. Baada ya kupitia hukumu na kuadibiwa kwa miaka kadhaa, wanakuja kuelewa bila kujua kusudi la usimamizi wa Mungu wa wanadamu na pia siri ya usimamizi Wake na wokovu wa wanadamu. Wanakuja kuelewa mapenzi ya Mungu na kujua ukuu Wake. Wanahisi kuwa wanaishi maisha yenye utajiri, amani, na maana. Mungu hukuruhusu uishi na ikiwa unaweza kuishi kwa ajili ya Mungu na kuishi ili kutekeleza wajibu wa kiumbe, basi unaishi maisha yenye maana. Ikiwa unaishi maisha ya maiti anayetembea, asiye na roho, kutokubali ukweli, unaishi kwa ajili ya mwili tu, basi huishi maisha yenye maana, kwani maisha yako hayana thamani.

2 Kati ya binadamu wote, ninyi ndinyi mliojaaliwa na kuteuliwa; mlizaliwa katika enzi hii, katika nchi ya joka kubwa jekundu, na Yeye huwaruhusu mtekeleze wajibu wenu wa sasa. Mmependwa na Mungu; mmechaguliwa na Yeye. Hii ni baraka. Mungu anawapenda na anawaruhusu mjitumie kwa ajili Yake, mtekeleze wajibu wenu katika familia ya Mungu, mtekeleza wajibu wa kiumbe, na kutoa sehemu ya bidii yenu. Hii sio baraka? Sasa mnaweza kuishi kila siku mkimshuhudia Mungu na kueneza injili ya ufalme wa Mungu; jambo hilo limeidhinishwa na Mungu.

3 Mungu anakupa fursa hii uishi kwa njia hii na kujitumia kwa ajili Yake—hili ni jambo la maana. Mnapaswa kuthamini fursa hii, na kuhisi fahari na heshima. Kuweza kutekeleza wajibu huu katika enzi hii, katika mazingira haya, na katika hali hizi ni fursa adimu sana! Mungu huchagua kwa uangalifu kutoka miongoni mwa binadamu, na amewachagua. Hii ni fursa yenu. Hii ni baraka yenu kubwa. Baraka hii ni kubwa zaidi kuliko baraka za watakatifu katika enzi zote na vizazi vyote!

Umetoholewa kutoka kwa ushirika wa Mungu

Iliyotangulia:Jinsi ya Kuchukulia Agizo la Mungu

Inayofuata:Tafuta Ukweli ili Uwe na Kazi ya Roho Mtakatifu

Maudhui Yanayohusiana

 • Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

  1 Kutoka unapoingia katika dunia hii ukilia, unaanza kutenda wajibu wako. Katika mpango na utaratibu wa Mungu, unachukua nafasi yako, na unaanza safar…

 • Kusudi la Kazi ya Mungu la Usimamizi

  1 Mungu ana mpango wa usimamizi wa miaka 6,000, uliyogawanywa katika hatua tatu, kila moja inaitwa enzi. Kwanza ni Enzi ya Sheria, kisha Enzi ya Neema…

 • Umuhimu wa Mungu Kumsimamia Binadamu

  Usimamizi wa Mungu ni ili kuwapata binadamu wanaomwabudu na kumtii Yeye. Ingawa wamepotoshwa na Shetani, hawamwiti baba tena, hawamwiti baba tena. 1 …

 • Upendo Safi Bila Dosari

  1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au vizuizi au ba…