554 Unaishi Katika Maneno ya Mungu kwa Kweli?

1 Muda unapita, na kufumba na kufumbua leo imefika. Chini ya uongozi wa Roho Wangu, watu wote wanaishi katikati ya mwanga Wangu, na hakuna anayefikiria yaliyopita ama kuiwekea jana maanani. Nani hajawahi kuishi katika wakati wa sasa? Ni nani ambaye hajapitia katika siku na miezi ya ajabu katika ufalme? Ni nani hajaishi chini ya jua? Ingawa ufalme umeshuka miongoni mwa mwanadamu, hakuna ambaye amepata kupitia ukunjufu wake; mwanadamu anautambua tu kutoka nje, bila kufahamu dutu lake.

2 Wakati ambapo ufalme Wangu unatengenezwa, ni nani asiyefurahi kwa sababu yake? Je, nchi katika dunia zinaweza kuutoroka kweli? Je, joka kubwa jekundu linaweza kutoroka kwa msaada wa ujanja wake? Amri Zangu za utawala zinatangazwa katika ulimwengu wote, zinaasisi mamlaka Yangu miongoni mwa watu wote, na zinatumika katika ulimwengu wote; hata hivyo, mwanadamu hajawahi kweli kuyafahamu haya. Wakati amri Zangu za utawala zinafichuliwa kwa ulimwengu ndipo pia wakati kazi Yangu duniani itakuwa karibu kukamilika. Nitakapotawala na kuonyesha nguvu miongoni mwa wanadamu wote na Nitakapotambulika kuwa Mungu mmoja Mwenyewe, ufalme Wangu utashuka duniani kikamilifu.

3 Leo, watu wote wana mwanzo mpya kwenye njia mpya. Wameanza maisha mapya, ilhali hakuna yule ambaye amewahi kwa kweli kuyapitia maisha duniani sawa na mbinguni. Je, mnaishi kweli katika mwanga Wangu? Je, mnaishi kweli miongoni mwa maneno Yangu? Ni nani asiyetilia maanani matarajio yake mwenyewe? Ni nani asiye na wasiwasi kuhusu hatima yake? Nani hapambani katika bahari ya mateso? Ni nani asiyetaka kujiweka huru? Je, baraka za ufalme ni kwa sababu ya bidii ya mwanadamu duniani? Je, tamaa zote za mwanadamu zinaweza kutimizwa jinsi anavyotaka?

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 25” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 553 Kutenda Ukweli Katika Wajibu Wako ni Muhimu

Inayofuata: 555 Watu Hawajampa Mungu Mioyo Yao Kabisa

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

83 Upendo wa Kweli

1 Namrudia Mungu na kuuona uso Wake upendezao, nikiwa huru kutokana na udhibiti wa kaida za dini. Neno Lake linanijaza na raha na furaha...

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki