714 Wale Walio na Mabadiliko ya Tabia Wanaweza Kuishi Kama Binadamu

1 Wale ambao wana mabadiliko katika tabia zao wanaishi kwa kudhihirisha sura ya binadamu kwa kweli, nao wana0 ukweli; hawategemei ushawishi wa wengine. Wale ambao wamekuwa na mabadiliko katika tabia wako imara zaidi, hawasitasiti, na haijalishi wako katika hali gani, wanajua jinsi ya kutimiza wajibu wao sawasawa na jinsi ya kufanya mambo ili kumridhisha Mungu. Wale ambao tabia zao zimebadilika hawalengi nini cha kufanya ili kujifanya waonekane wazuri katika kiwango cha juujuu—wanao uwazi wa ndani kuhusu kile cha kufanya ili kumridhisha Mungu. Kwa hivyo, kutoka nje wanaweza kukosa kuonekana wenye shauku sana ama kama wamefanya jambo lolote kubwa, lakini kila kitu wanachofanya kina maana, kina thamani, na kina matokeo ya kiutendaji.

2 Wale ambao tabia zao zimebadilika wana uhakika kuwa na ukweli mwingi—hii inaweza kuthibitishwa kwa mitazamo yao kuhusu mambo na kanuni zao katika vitendo vyao. Wale wasio na ukweli hawajakuwa na mabadiliko yoyote katika tabia hata kidogo. Bila shaka, mabadiliko katika tabia yanajumuisha hali hizi, lakini jambo lililo muhimu zaidi ni kuwa maisha yao ya ndani yamebadilika. Ukweli unaoonyeshwa na Mungu unakuwa maisha yao hasa, baadhi ya sumu za kishetani zilizo ndani zimetolewa, mitazamo yao imebadilika kabisa, na hakuna kati ya hiyo inakubaliana na ile ya dunia. Anaona waziwazi njama na sumu za joka kubwa jekundu; amefahamu kiini cha kweli cha maisha. Kwa hivyo maadili ya maisha yake yamebadilika—hili ndilo badiliko la muhimu zaidi na kiini cha mabadiliko katika tabia.

3 Hata hivyo, wale walio na mabadiliko katika tabia wako tofauti. Jinsi wanavyopaswa kuishi maisha ya maana, jinsi wanavyopaswa kutimiza wajibu wa mtu ili wastahili kuitwa wanadamu, jinsi wanavyopaswa kumwabudu Mungu, na jinsi wanavyopaswa kumtii na kumridhisha Mungu—wanaamini kwamba huu ndio msingi wa kuwa mtu na ni wajibu wao kulingana na kanuni zisizobadilika za Mbinguni na dunia. Vinginevyo, hawangestahili kuitwa wanadamu: maisha yao yangekuwa matupu na yasiyo na maana. Wanahisi kwamba watu wanafaa kuishi ili kumridhisha Mungu, kutimiza wajibu wao vizuri, na kuishi maisha yenye maana, ili hata watakapokufa, watahisi kuridhika na hawatakuwa na majuto yoyote—hawatakuwa wameishi bure. Kwa hiyo, chanzo kikuu cha mabadiliko katika tabia ya maisha ya mtu ni kuwa na ukweli kwa ndani, na kuwa na maarifa kuhusu Mungu; mtazamo wa mtu wa maisha unabadilika, na maadili ni tofauti na awali. Mabadiliko yanaanza kutoka ndani, na kutoka kwa maisha ya mtu; kwa kweli si tu mabadiliko ya nje.

Umetoholewa kutoka katika “Tofauti Kati Ya Mabadiliko Ya Nje Na Mabadiliko Katika Tabia” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 713 Sifa za Mabadiliko ya Tabia

Inayofuata: 715 Huu ni Mfano wa Mtu halisi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp