257 Maisha ya Viumbe Wote Yatoka kwa Mungu

1 Kwamba uzima aliopewa mwanadamu na Mungu hauna mipaka, na hauzuiliwi na maumbile ya nje, wakati, au nafasi. Hili ndilo fumbo la uzima aliopewa binadamu na Mungu, na dhihirisho kwamba maisha yalikuja kutoka Kwake. Ingawa watu wengi wanaweza kukosa kuamini kwamba maisha yalitoka kwa Mungu, binadamu bila ya kufahamu hufurahia yote yatokayo kwa Mungu, iwe wanaamini au wanakana uwepo Wake. Iwapo siku moja Mungu kwa ghafla Atabadili moyo na Atake kurudisha yote yaliyomo duniani na kuchukua maisha Aliyotoa, basi yote duniani yataisha.

2 Mungu hutumia maisha Yake kukimu vitu vyote vilivyo hai na visivyo na uhai, na kuleta yote kwa utaratibu mzuri kwa mujibu wa uwezo na mamlaka Yake. Huu ni ukweli ambao hauwezi kuwazika au kueleweka na yeyote, na kweli hizi zisizoeleweka kwa fikira zetu ni dhihirisho halisi na ushahidi wa nguvu za Mungu katika maisha. Sasa hebu nikupe siri: Ukuu wa uzima wa Mungu na nguvu ya uzima Wake haziwezi kueleweka na kiumbe yeyote. Hivi ndivyo hali ilivyo sasa, kama ilivyokuwa awali, na itakuwa hivyo wakati ujao.

3 Siri ya pili Nitakayotoa ni hii: Chanzo cha uhai hutoka kwa Mungu, kwa viumbe wote, bila kujali jinsi wanavyoweza kuwa tofauti katika maumbile au muundo. Hata uwe kiumbe hai wa aina gani, huwezi kwenda kinyume na njia ya maisha ambayo Mungu ameweka. Katika hali yoyote, kile Napenda ni kuwa mwanadamu kuelewa hili: Bila ulinzi, utunzaji, na utoaji wa Mungu, mwanadamu hawezi kupokea yote aliyokusudiwa kupokea, haijalishi anajaribu kwa juhudi au kupambana kwa bidii namna gani. Bila ruzuku ya uhai kutoka kwa Mungu, mwanadamu hupoteza maana ya thamani ya kuishi na madhumuni ya maana katika maisha.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 256 Jinsi Mungu Anavyotawala Vitu Vyote

Inayofuata: 258 Mfano Halisi wa Nguvu Uzima ya Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp