Tunawakaribisha wote wanaotafuta ukweli wawasiliane nasi.

Mfuateni Mwanakondoo na Kuimba Nyimbo Mpya

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

(Ma)tokeo ya Kutafuta 0

Hakuna matokeo yaliyopatikana

280 Upendo Hukesha

Umepata mwili na Unaonyesha ukweli ili kuwaokoa wanadamu.

Maneno Yako yote ni ukweli, huiamsha mioyo ya wanadamu.

Unakesha mchana na usiku, nasi kila wakati katika upepo na mvua.

Umemwaga damu ya moyo Wako ili wanadamu waweze kuokolewa.

Unavumilia uasi na kuelewa kwetu vibaya bila malalamiko au majuto.

Lakini ni watu wangapi wanaelewa moyo Wako?

Na ni wangapi wamegutuka na kukupa mioyo yao?

Una wasiwasi mwingi sana, mashaka na kutanafusi kwingi sana.

Ugumu na uchungu mwingi sana, Unavumilia mambo haya yote peke Yako.

Maneno Yako huhukumu na kuwafunua watu, na hufichua upendo Wako.

Umepata aibu kubwa ili kuwaokoa wanadamu.

Ni miaka mingapi ya kukesha? Ni miaka mingapi ya kungojea?

Ni kwa ajili tu ya kupata kikundi cha watu wanaokupenda kwa dhati.

Makusudi Yako ya fadhila na upendo Wako wa dhati

vimeurudishia moyo wangu uliokufa ganzi uzima.

Ningewezaje kuwa mwasi tena? Ningewezaje kufa moyo au kurudi nyuma tena?

Umetumaini, Umesubiri muda mrefu sana tayari.

Ningewezaje kuvumilia kukuacha Usubiri tena, kukuumiza zaidi?

Kwenye mkondo huu wa mwisho, natamani kukufuata nyuma Yako kwa karibu, bila kukoma.

Niko tayari kufanya yote niwezayo kufuatilia ukweli ili nipate ukweli na uzima.

Haijalishi mateso na shida zilivyo kubwa na kali, nimeamua kabisa kukufuata.

Kuweza kukupenda, kuwa shahidi mzuri Kwako ni hamu ya moyo wangu katika maisha haya.

Iliyotangulia:Upendo wa Kweli Miongoni mwa Binadamu

Inayofuata:Mungu Bado Anatupenda Leo

Maudhui Yanayohusiana