770 Mungu Atumai Kwamba Mwanadamu Ampende Mungu kwa Moyo, Akili na Nguvu Zake Zote

1 Mungu karibu amemaliza kazi Yake ndani ya watu wa kanisa, baadaye Atatumia ghadhabu kuonekana mbele ya watu wote. Kazi hii lazima itekelezwe kwa njia ya Mungu kusababisha mabaa mbalimbali duniani. Lakini Mungu hataonekana. Katika wakati huu, vyote vinavyoishi katika taifa la joka kubwa jekundu vitapitia maafa, ambavyo kwa kawaida ni pamoja na ufalme ulio duniani (kanisa). Huu ndio hasa wakati ambao ukweli hujitokeza, na kwa hiyo unapitiwa na watu wote, na hakuna anayeweza kuepuka. Hili limejaaliwa na Mungu. Na kwa ajili ya majilio ya machafuko, watu wataweza tu kufikiria kuhusu kile kilicho mbele yao na watapuuza kila kitu kingine, na ni vigumu kwao kumfurahia Mungu katikati ya machafuko, hivyo, watu wanatakiwa kumpenda Mungu kwa moyo wao wote katika wakati huu wa ajabu, ili wasikose nafasi.

2 Ukweli huu unapopita, Mungu amelishinda kabisa joka kubwa jekundu, na hivyo kazi ya ushuhuda wa watu wa Mungu imefika mwisho; baadaye Mungu ataanza hatua inayofuata ya kazi, Akifanya uharibifu kwa nchi ya joka kubwa jekundu, na hatimaye kuwagongomelea watu juu chini msalabani kotekote katika ulimwengu, baadaye Atawaangamiza wanadamu wote—hizi ni hatua za siku za baadaye za kazi ya Mungu. Hivyo, mnapaswa kutaka kufanya lote muwezalo kumpenda Mungu katika mazingira haya ya amani. Katika siku za baadaye hamtakuwa na nafasi zaidi za kumpenda Mungu, kwani watu huwa tu na nafasi ya kumpenda Mungu katika mwili; wanapoishi katika ulimwengu mwingine, hakuna atakayenena kuhusu kumpenda Mungu. Je, hili si jukumu la kiumbe aliyeumbwa?

3 Kwa hiyo unapaswa kumpenda Mungu vipi katika siku zako za uhai? Umeshawahi kufikiri juu ya hili? Je, unangoja mpaka ufe ili umpende Mungu? Je, haya si maneno matupu? Leo, kwa nini hufuatilii kumpenda Mungu? Inatarajiwa kwamba mnaweza kumpenda Mungu kwa mioyo yenu yote, kwa akili zenu zote, na kwa nguvu zenu zote, jinsi tu mnavyotunza maisha yenu wenyewe. Je, haya siyo maisha yenye maana kuu zaidi? Ni wapi pengine ambapo mngeweza kupata maana ya maisha? Je, ninyi si vipofu kabisa? Uko radhi kumpenda Mungu? Kwa hiyo, unapaswa kufanya nini? Mpende Mungu kwa ujasiri, bila kusita.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 42” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 769 Wale Wanaompenda Mungu Wana Nafasi ya Kukamilishwa

Inayofuata: 771 Mungu Awalinda Wale Wampendao

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp