68 Lengo Kuu la Kazi ya Mungu ya Ushindi

1 Shabaha kuu ya kazi ya kushinda ni kuwatakasa binadamu ili mwanadamu aweze kuwa na ukweli, kwa sababu mwanadamu sasa anauelewa ukweli kidogo sana! Kufanya kazi ya kushinda kwa watu hawa ni jambo la umuhimu mkubwa mno. Nyote mmeanguka katika ushawishi wa giza na mmeumizwa mno. Shabaha ya kazi hii, basi, ni kuwawezesha kujua asili ya binadamu na hivyo basi kuishi kwa ukweli. Kama unaweza kutoroka ushawishi huu wa giza na kujitenga na mambo hayo machafu, kama unaweza kuwa mtakatifu, inamaanisha kwamba unao ukweli. Si kwamba asili yako yamebadilika, lakini tu kwamba unaweza kuweka ukweli katika matendo na unaweza kuunyima mwili wako. Haya ndiyo yanayopatikana kwa wale waliotakaswa.

2 Ni wale tu walio na ukweli na wanaoishi ukweli wanaoweza kumilikiwa kabisa na Mungu. Yaani, wale wanaoishi kwa kudhihirisha mfano wa Petro ndio wanaofanywa kuwa wakamilifu, huku wengine wote ndio ambao wameshindwa. Kazi inayofanywa kwa wale wote wanaoshindwa inajumuisha tu kuweka laana, kuadibu, na kuonyesha hasira, na yale yanayowajia ni haki na laana tu. Kushughulikia mtu kama huyo ni kufichua waziwazi—kufichua tabia potovu iliyo ndani yake ili aweze kuitambua mwenyewe na kushawishika kabisa. Punde binadamu anapokuwa mtiifu kabisa, kazi ya ushindi inakamilika. Hata kama watu wengi wangali hawatafuti kuelewa ukweli, kazi ya ushindi itakuwa imekamilika.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Waliokamilishwa Pekee Ndio Wanaoweza Kuishi Maisha Yenye Maana” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 67 Hatua ya Mwisho ya Ushindi Inakusudiwa Kuwaokoa Watu

Inayofuata: 69 Umuhimu wa Kazi ya Ushindi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp