731 Mwanadamu Atoa Mahitaji Mengi Sana kwa Mungu
1 Mantiki ya watu ina dosari sana, na wana mahitaji mengi mno kwa Mungu, ambayo ni mengi kupita kiasi; hawana mantiki. Watu daima wamekuwa wakimtaka Mungu kufanya mambo kwa njia hii na kwa njia ile. Wameshindwa kabisa kumtii Mungu au kumwabudu. Badala yake, wao huja na maombi yao yasiyo na busara kulingana na matamanio yao wenyewe; wao humwomba Mungu awe na uvumilivu mwingi, asiwe na hasira juu ya chochote, daima kuwaangalia kwa tabasamu kwenye uso Wake. Bila kujali wakati, Mungu lazima azungumze daima, daima Aizuie hasira Yake, na kuonyesha maneno mazuri kwao. Mnapaswa kutafakari juu ya mambo haya. Je, si mantiki ya binadamu ina dosari sana? Siyo tu kwamba wameshindwa kuitii kabisa mipango na mipangilio ya Mungu au kukubali kila kitu kutoka kwa Mungu, lakini kinyume chake wao hulazimisha mahitaji mengine ya ziada kwa Mungu. Watu wanawezaje kuwa waaminifu kwa Mungu ikiwa wana mahitaji ya aina hii? Wanawezaje kuitii mipango ya Mungu? Ikiwa watu wana aina hizi za mahitaji, basi wanawezaje kumpenda Mungu?
2 Watu wote wana mahitaji ya jinsi Mungu anastahili kuwapenda, kuwavumilia, kuwaangalia na kuwalinda, na kuwatunza, lakini hawana mahitaji ya wao wenyewe ya jinsi ya kumpenda Mungu, jinsi ya kumfikiria Mungu, jinsi ya kumwangalia Mungu, jinsi ya kumridhisha Mungu, jinsi ya kuwa na Mungu mioyoni mwao, na jinsi ya kumwabudu Mungu. Je, vitu hivi vimo katika mioyo ya watu? Hivi ni vitu ambavyo watu wanapaswa kufanya, hivyo kwa nini watu hawasongi mbele kwa bidii katika vitu hivi? Watu wengine wana shauku kwa muda, lakini si ya kudumu; wakikumbana na kipingamizi kidogo, kinaweza kuwasababisha wakose tumaini na kulalamika. Watu wana shida nyingi zaidi na kuna watu wachache sana ambao huutafuta ukweli na hutaka kumpenda na kumridhisha Mungu. Watu hasa ni muhali na hawasimami kwa usahihi katika nafasi zao. Aidha, wao hujiona kuwa muhimu kwa namna ya pekee.
Umetoholewa kutoka katika “Watu Ambao Hufanya Madai Daima kwa Mungu Ndio Wenye Busara Kidogo Zaidi” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo