138 Lazima Mwanadamu Amshuhudie Mungu Katika Kila Hatua ya Kazi Yake

1 Usimamizi mzima wa Mungu umegawika katika hatua tatu, na katika kila hatua, mahitaji yanayofaa yanatakiwa kutoka kwa mwanadamu. Aidha, kadri enzi zinavyopita na kuendelea, mahitaji ya Mungu kwa wanadamu wote huwa ya juu hata zaidi. Kwa hiyo, hatua kwa hatua, kazi hii ya usimamizi wa Mungu hufikia kilele chake, hadi mwanadamu aamini ukweli wa “kuonekana kwa Neno katika mwili,” na kwa njia hii mahitaji ya mwanadamu huwa ya juu hata zaidi, na mahitaji ya mwanadamu kutoa ushuhuda huwa ya juu hata zaidi. Kadiri mwanadamu alivyo na uwezo wa kushirikiana na Mungu kwa kweli, ndivyo anavyozidi kumtukuza Mungu. Ushirikiano wa mwanadamu ndio ushuhuda anaohitajika kuwa nao, na ushuhuda alio nao ndio matendo ya mwanadamu.

2 Wakati wa kale, mwanadamu alihitajika kutii sheria na amri, na alihitajika kuwa mwenye subira na mnyenyekevu. Leo, mwanadamu anahitajika kutii mipango yote ya Mungu na awe na upendo mkuu wa Mungu, na hatimaye bado anahitajika kumpenda Mungu katika taabu. Hatua hizi tatu ndizo Mungu anazozitazamia kutoka kwa mwanadamu, hatua kwa hatua, katika usimamizi Wake wote. Kila hatua ya kazi ya Mungu huzidisha kina kuliko iliyopita, na katika kila hatua, mahitaji kwa mwanadamu ni makubwa kuliko yaliyopita, na kwa njia hii, usimamizi mzima wa Mungu huonekana. Ni hasa kwa sababu mahitaji ya mwanadamu kila mara huwa ya juu kiasi kwamba tabia yake kila mara inafikia viwango anavyovihitaji Mungu, na ni hapo tu ambapo wanadamu wote wanaanza kujiondoa polepole kutoka kwa ushawishi wa Shetani hadi, ambapo kazi ya Mungu itafikia kikomo kabisa, ndio wanadamu wote watakuwa wameokolewa kutoka kwa ushawishi wa Shetani.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu na Utendaji wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 137 Kazi Yote ya Mungu ni ya Vitendo Kabisa

Inayofuata: 139 Tofauti Kati ya Kazi ya Mungu na Kazi ya Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp