281 Binadamu Hawawezi Kudhibiti Majaliwa Yao Wenyewe

1 Pale utakapoenda kila siku, kile utakachofanya, yule au kile utakachokumbana nacho, kile utakachosema, kile kitakachokufanyikia—je, kati ya vyote hivi kipo kinachoweza kutabirika? Watu hawawezi kutabiri matukio haya yote, sikutajii kudhibiti namna ambavyo yanavyoendelea. Katika maisha, matukio haya yasiyotabirika hufanyika kila wakati, na ni tukio la kila siku. Mabadiliko haya ya kila siku na njia ambazo yanajitokeza, au ruwaza ambazo yanajitokeza, ni vikumbusho vya kila wakati kwa binadamu kwamba hakuna kinachofanyika bila mpango, kwamba njia ya maendeleo inayochukuliwa na mambo haya, na kutoepukika kwa mambo haya, haviwezi kubadilishwa na mapenzi ya binadamu.

2 Kila tukio linaonyesha onyo kutoka kwa Muumba kwa mwanadamu, na pia linatuma ujumbe kwamba, binadamu hawawezi kudhibiti hatima zao wenyewe; na wakati uo huo kila tukio ni upingaji wa malengo yasiyo na mwelekeo, yasiyo na maana ya binadamu na tamanio la kuchukua hatima yake na kutaka kuidhibiti mwenyewe. Ni sawa na makofi yenye nguvu juu ya masikio ya binadamu moja baada ya jingine, yanayolazimisha binadamu kufikiria upya ni nani, hatimaye, atatawala na kudhibiti hatima yao. Na kama vile malengo na matamanio yao yanavyokiukwa mara kwa mara na kusambaratika, binadamu kwa kawaida huishia kukubali kwa nadharia yao bila kufahamu kile ambacho hatima yao imesheheni, kukubali kwa uhalisi, kwa mapenzi ya Mbinguni na ukuu wa Muumba.

Kutokana na mabadiliko haya ya kila siku katika hatima za maisha yote ya binadamu, hakuna kitu ambacho hakifichui mipango ya Muumba na ukuu Wake; hakuna kile ambacho hakiutumi ujumbe huu kwamba “yale mamlaka ya Muumba hayawezi kupitwa,” ambacho hakionyeshi ukweli wa milele kwamba “mamlaka ya Muumba ni ya juu zaidi.”

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee III” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 280 Mungu Ndiye Mkuu wa Pekee wa Majaliwa ya Mwanadamu

Inayofuata: 282 Mungu Aliamua Majaliwa ya Mwanadamu Kitambo

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp