169 Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili

1 Mungu alifanyika mwili kwa sababu lengo la kazi Yake si roho ya Shetani, au kitu chochote kisicho cha mwili, ila mwanadamu, ambaye ni wa mwili na ambaye amepotoshwa na Shetani. Ni kwa sababu hii hasa kwamba mwili wa mwanadamu umepotoshwa ndiyo maana Mungu amemfanya mwanadamu mwenye mwili kuwa mlengwa wa kazi Yake; aidha, kwa sababu mwanadamu ni mlengwa wa upotovu, Amemfanya mwanadamu kuwa mlengwa wa pekee wa kazi Yake katika hatua zote za kazi Yake ya wokovu. Mwanadamu ni kiumbe anayekufa, ni wa mwili na damu, na Mungu ndiye tu Anayeweza kumwokoa mwanadamu. Kwa namna hii, ni lazima Mungu awe mwili ambao una tabia zinazofanana na mwanadamu ili Aweze kufanya kazi Yake, ili kwamba kazi Yake iweze kupata matokeo mazuri zaidi. Mungu lazima awe mwili ili Aweze kufanya kazi Yake kwa ufanisi kwa sababu mwanadamu ni wa mwili, na hana uwezo wa kushinda dhambi au kujivua mwili.

2 Mungu anapofanya kazi katika mwili, kwa hakika Anapambana na Shetani katika mwili. Anapofanya kazi katika mwili, Anafanya kazi Yake katika ulimwengu wa kiroho, na Anafanya kazi Yake yote katika ufalme wa kiroho ili iwe halisi duniani. Anayeshindaniwa ni mwanadamu, asiye mtiifu Kwake, yule anayeshindwa ni mfano halisi wa Shetani (bila shaka, huyu pia ni mwanadamu), ambaye ana uadui na Yeye, na ambaye ataokolewa hatimaye ni mwanadamu. Kwa namna hii, ni muhimu zaidi Kwake kuwa mwanadamu ambaye ana ganda la nje la kiumbe, ili kwamba Awe na uwezo wa kupambana na Shetani katika uhalisi, kumshinda mwanadamu, ambaye si mtiifu Kwake na ambaye ana kuonekana kwa nje ambako kunafanana na Yeye, na kumwokoa mwanadamu, ambaye ana umbo la nje kama Lake na aliyeumizwa na Shetani. Adui Wake ni mwanadamu, mlengwa wa ushindi Wake ni mwanadamu, na mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, aliyeumbwa na Yeye. Hivyo ni lazima Awe mwanadamu, na kwa njia hii, kazi Yake inakuwa rahisi zaidi. Ana uwezo wa kumshinda Shetani na kumshinda mwanadamu, aidha, anaweza kumwokoa mwanadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 168 Kristo wa Siku za Mwisho Ndiye Mlango wa Mwanadamu Kuingia Katika Ufalme

Inayofuata: 170 Kupata Mwili Kote Kuwili kwa Mungu Kunahitajika na Binadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp