361 Udanganyifu wa Mwanadamu kwa Mungu Huenea Katika Matendo Yao

1 Watu wengi wangependa kunipenda kwa kweli, lakini kwa sababu mioyo yao si yao wenyewe, hawawezi kujidhibiti wenyewe; watu wengi hunipenda kwa kweli katika majaribio Ninayotoa, lakini hawana uwezo wa kuelewa kwamba Mimi kwa kweli Nipo, na wananipenda tu katikati ya utupu; na si kwa sababu ya kuwepo Kwangu halisi; watu wengi, baada ya kuweka nyoyo zao mbele Zangu, hawazijali, na hivyo nyoyo zao zinanyakuliwa na Shetani wakati wowote anapopata nafasi, na baada yake huniacha; watu wengi hunipenda kwa dhati Ninapotoa maneno Yangu, lakini hawathamini maneno Yangu katika roho zao, badala yake wakiyatumia kwa kawaida kama mali ya umma na kuyatupa yalipotoka wakati wowote wanapotaka.

2 Mwanadamu hunitafuta akiwa na maumivu, na hunitazamia akiwa na majaribu. Wakati kuna amani yeye hunifurahia, wakati wa hatari yeye hunikana, wakati ana kazi nyingi yeye hunisahau, na asipokuwa na kitu cha kufanya yeye hufanya vitu kwa namna isiyo ya dhati—lakini kamwe hakuna yeyote ambaye amenipenda katika maisha yake yote. Ningependa mwanadamu awe mwenye bidii mbele Zangu: Mimi Simuombi chochote, ila tu watu wote wanichukulie kwa umakini, kwamba, badala ya kunirairai, waniruhusu kurudisha uaminifu wa mwanadamu.

3 Nuru Yangu, mwangaza na gharama ya juhudi Zangu huenea kwa watu wote, ilhali hivyo pia ukweli halisi wa kila tendo la mwanadamu huenea kwa watu wote, kama ufanyavyo wao kunidanganya. Sijawahi kuchanganywa na ushawishi na hila za mwanadamu, kwa maana Mimi Nilishatambua kiini chake muda mrefu uliopita. Nani anayejua kiasi cha uchafu ulio katika damu yake, na kiasi gani cha sumu ya Shetani kimo ndani ya mafupa yake? Mwanadamu anapata uzoefu wa sumu hii kila uchao, hata anakosa busara ya kufahamu maafa ya Shetani na hivyo hana nia ya kutambua “sanaa ya uwepo wa afya.”

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 21” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 360 Unaishi Katika Maneno ya Mungu kwa Kweli?

Inayofuata: 362 Mungu Hamruhusu Kiumbe Yeyote Kumdanganya

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp