299 Tabia ya Mwanadamu Imekuwa ya Katili Sana

1 Baada ya miaka elfu kadhaa ya upotovu, mwanadamu amekuwa asiyehisi na mpumbavu, pepo anayempinga Mungu, kwa kiasi kwamba uasi wa mwanadamu kwa Mungu umeandikwa katika vitabu vya historia, na hata mwanadamu mwenyewe hana uwezo wa kutoa ripoti kamili ya tabia zake za uasi wake—kwa kuwa mwanadamu amepotoshwa sana na Shetani, na amehadaiwa na Shetani kiasi kwamba hajui ni wapi pa kugeukia. Hata wa leo, mwanadamu bado anamsaliti Mungu: Wakati mwanadamu anamwona Mungu, anamsaliti, na wakati yeye hawezi kumwona Mungu, bado anamsaliti. Kuna hata wale ambao, baada ya kushuhudia laana ya Mungu na ghadhabu ya Mungu, bado wanamsaliti. Na hivyo Nasema kwamba hisia ya mwanadamu imepoteza kazi yake ya awali, na kwamba dhamiri ya mwanadamu, pia, imepoteza kazi yake ya awali. Mwanadamu Ninayemtazamia ni mnyama katika mavazi ya binadamu, yeye ni nyoka mwenye sumu.

2 Tabia ya mwanadamu imekuwa mbaya zaidi, akili yake imekuwa hafifu zaidi, na dhamiri yake imekanyagwa kabisa na yule muovu na kwa muda mrefu imekoma kuwa dhamiri ya awali ya mwanadamu. Mwanadamu hajakosa tu shukrani kwa Mungu mwenye mwili kwa kukabidhi maisha na neema nyingi juu ya wanadamu, bali pia anachukia Mungu kwa kumpatia ukweli; ni kwa sababu mwanadamu hana haja ya kujua ukweli hata kidogo ndio maana anamchukia Mungu. Haitoshi kwamba mwanadamu hawezi kuutoa uhai wake kwa ajili ya Mungu mwenye mwili tu, lakini pia anajaribu kutoa neema kutoka kwa Mungu, na anafanya madai kwa Mungu yaliyo mara kadhaa kubwa kuliko kile mwanadamu ametoa kwa Mungu. Watu wa dhamiri na hisia kama hizo hufikiria kwamba hili si jambo kubwa, na bado wanaamini kuwa wao wamefanya mengi sana kwa ajili ya Mungu, na kwamba Mungu amewapa kidogo sana. Ukiwa na ubinadamu kama huo, na dhamiri ya aina hii, ni jinsi gani bado mnatarajia kupata uzima? Nyinyi ni fukara wa kudharauliwa mlioje!

Umetoholewa kutoka katika “Kuwa na Tabia Isiyobadilika Ni Kuwa katika Uadui na Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 298 Ukweli wa Matokeo ya Kupotoshwa kwa Mwanadamu na Shetani

Inayofuata: 300 Watu Waishio Katika Nchi Chafu Sana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp