378 Usaliti ni Asili ya Mwanadamu

1 Asili ya mwanadamu ni tofauti kabisa na kiini Changu, kwa sababu asili potovu ya mwanadamu hutoka kwa Shetani kabisa; asili ya mwanadamu imetengenezwa na kupotoshwa na Shetani. Yaani, mwanadamu anaishi chini ya ushawishi wa uovu na ubaya wake. Mwanadamu hakui katika ulimwengu wa ukweli au mazingira matakatifu, sembuse mwanadamu kuishi katika nuru. Kwa hiyo, haiwezekani kwa mtu yeyote kuwa na ukweli ndani ya asili yake tangu wakati wa kuzaliwa, sembuse mtu kuweza kuzaliwa na kiini kinachomwogopa na kumtii Mungu. Badala yake, watu wana asili ambayo humpinga na kumwasi Mungu, na haipendi ukweli. Asili hii ndilo tatizo Ninalotaka kujadili—usaliti.

2 Msingi wa uwepo wa wanadamu ni kuzaliwa upya kwa nafsi tena na tena. Kwa maneno mengine, kila mtu hupata maisha ya kibinadamu katika mwili nafsi yake inapozaliwa upya. Baada ya mwili wa mtu kuzaliwa, maisha yake huendelea hadi mwili unapofikia vikomo vyake hatimaye, ambao ndio wakati wa mwisho, wakati nafsi inapoliacha ganda lake. Utaratibu huu hujirudia tena na tena, nafsi ya mtu ikija na kwenda mara kwa mara, na kwa hiyo uwepo wa wanadamu unadumishwa. Maisha ya mwili pia ni maisha ya nafsi ya mwanadamu, na nafsi ya mwanadamu hukimu uwepo wa mwili wa mwanadamu. Hiyo ni kusema, maisha ya kila mtu hutoka kwenye nafsi yake, na maisha hayana asili katika mwili. Kwa hiyo, asili ya mwanadamu hutoka kwenye nafsi, si kutoka kwa mwili.

3 Nafsi ya kila mtu tu ndiyo inayojua jinsi alivyopitia majaribu, mateso na upotovu wa Shetani. Mwili wa mwanadamu hauyajui mambo haya. Kwa hiyo, bila kujua, wanadamu huwa waovu zaidi, wachafu zaidi, na wabaya zaidi, wakati umbali kati ya mwanadamu na Mimi unazidi kuwa mkubwa, na maisha yanakuwa yenye giza zaidi kwa wanadamu. Shetani huzishika nafsi za wanadamu kwa nguvu, kwa hiyo, bila shaka, mwili wa mwanadamu pia umemilikiwa na Shetani. Mwili kama huo na wanadamu kama hao wangewezaje kutompinga Mungu? Wangewezaje kulingana naye kiasili? Sababu iliyofanya Nimtupe Shetani chini angani ni kwa sababu alinisaliti. Je, basi wanadamu wanawezaje kutohusishwa? Hii ndiyo sababu usaliti ni asili ya kibinadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Tatizo Zito Sana: Usaliti (2)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 377 Matokeo ya Wale Wanaomwamini Mungu Lakini Wanamwasi

Inayofuata: 379 Kumsaliti Mungu ni Asili ya Binadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp