952 Uasi wa Mwanadamu Unaibua Hasira ya Mungu
1 Wakati hasira Yangu ya ghadhabu inapotingiza milima na mito, Sitamtawaza mwanadamu aina mbalimbali za msaada, kwa sababu ya woga wake. Wakati huu, Nitakuwa na ghadhabu, Nikiwanyima viumbe hai fursa ya kutubu na, kuachana na matumaini Yangu yote kwa mwanadamu, Nitatoa adhabu anayostahili sana. Wakati huu, radi na umeme vinang’aa ghafla na kunguruma, kama mawimbi ya bahari yakisonga kwa hasira, kama milima makumi ya maelfu ikigonga chini. Kwa ajili ya uasi wake, mwanadamu anaangushwa na radi na umeme, viumbe wengine wanafutwa katika milipuko ya radi na umeme.
2 Ulimwengu mzima unazorota ghafla katika machafuko, na uumbaji huwezi kupata pumzi muhimu ya uhai. Majeshi lukuki ya binadamu hayawezi kutoroka kishindo cha radi, katikati ya nuru ya ghafla ya umeme, wanadamu, makundi mengi sana, wanaanguka ndani ya mto unaobubujika haraka, kutokomezwa na mafuriko yanayotiririka chini kutoka milima. Ghafla, panakutana dunia ya “wanadamu” badala ya hatima ya binadamu. Maiti wanasongasonga juu ya bahari. Binadamu wote wanaenda mbali nami kwa sababu ya ghadhabu Yangu, kwani mwanadamu ametenda dhambi dhidi ya kiini cha Roho Wangu, uasi wake umenikosea Mimi. Lakini, mahali ambapo hakuna maji, wanadamu wengine bado wanafurahia, wakicheka na kuimba, ahadi ambazo Nimewapa.
Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 17” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili