235 Fikira za Mwanadamu ni za Kushikilia Ukale

1 Kazi ya Mungu inaendelea kusonga mbele, na ingawa madhumuni ya kazi Yake bado hayajabadilika, njia anazozitumia kufanya kazi zinabadilika mara kwa mara, na hivyo pia wale wanaomfuata Mungu. Zaidi iwapo kazi ya Mungu, zaidi mwanadamu anakuja kumjua kwa kina Mungu, na tabia ya mwanadamu inabadilika ipasavyo pamoja na kazi Yake. Hata hivyo, ni kwa sababu kazi ya Mungu milele inabadilika ndio wale wasiojua kazi ya Roho Mtakatifu na wale wanadamu wajinga wasiojua ukweli wanakuwa wapinzani wa Mungu. Kazi ya Mungu kamwe haifuati dhana za mwanadamu, kwani kazi Yake daima ni mpya na siyo nzee. Kamwe Hairudii kazi ya zamani lakini badala Anasonga mbele na kazi ambayo haijafanywa hapo awali.

2 Kwa sababu Mungu harudii kazi Yake na mwanadamu daima anahukumu kazi ya Mungu leo kulingana na kazi Yake ya zamani, ni vigumu sana kwa Mungu kutekeleza kila hatua ya kazi ya enzi mpya. Mwanadamu ana vizuizi vingi sana! Kufikiria kwa mwanadamu ni kwa akili finyu! Hakuna mwanadamu anayeijua kazi ya Mungu, lakini bado wote wanafafanua kazi hiyo. Mbali na Mungu, mwanadamu anapoteza uhai, ukweli na baraka za Mungu, lakini bado mwanadamu hajapokea uhai wala ukweli, na hata baraka kubwa Mungu anazowapa wanadamu. Wana maoni kwamba Mungu anaweza tu kuwa Mungu chini ya sheria na Mungu aliyesulubiwa kwa sababu ya mwanadamu; pia ni maoni yao kwamba Mungu hastahili na Hawezi kuzidi kiwango cha Biblia. Ni hasa maoni haya yaliyowafunga imara kwa sheria ya zamani na kuendelea kuwafumba kwa kanuni ngumu.

3 Hata zaidi wanaamini kwamba kazi yoyote ile mpya ya Mungu, ni lazima ithibitishwe na unabii, na kwamba katika kila hatua ya hiyo kazi, wote wanaomfuata na roho ya kweli lazima pia waonyeshwe ufunuo, vinginevyo kazi hiyo haiwezi kuwa ya Mungu. Tayari si kazi rahisi kwa mwanadamu kuja kumjua Mungu. Ikichukuliwa pamoja na moyo wa ujinga wa mwanadamu na asili yake ya kuasi ya kujiona muhimu na kujivunia, basi ni vigumu zaidi kwa mwanadamu kukubali kazi mpya ya Mungu. Mwanadamu haitafiti kazi mpya ya Mungu kwa utunzaji wala haikubali na unyenyekevu; badala yake, mwanadamu anachukua mtazamo wa dharau, kusubiri ufunuo na mwongozo wa Mungu. Hii siyo tabia ya mwanadamu anayeasi dhidi ya na kumpinga Mungu? Ni jinsi gani wanadamu kama hawa wanaweza kupata idhini ya Mungu?

Umetoholewa kutoka katika “Ni Jinsi Gani Ambavyo Mwanadamu Ambaye Amemwekea Mungu Mipaka katika Fikira Zake Anaweza Kupokea Ufunuo wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 234 Waumini wa Mungu Wanapaswa Kutafuta Mapenzi Yake ya Sasa

Inayofuata: 236 Wale Wasioikubali Kazi Mpya ya Roho Mtakatifu Wanaweza Kuona Kuonekana kwa Bwana?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp