673 Maana ya Majaribio na Usafishaji wa Mungu wa Mwanadamu

1 Kusudi la kazi ya usafishaji kimsingi ni ya kukamilisha imani ya watu. Mwishowe, kile kinachofanikishwa ni kwamba unataka kuondoka lakini, wakati huo huo, huwezi; baadhi ya watu bado wanaweza kuwa na imani hata wakati wanaondolewa hata chembe kidogo cha matumaini; na watu hawana tena tumaini kabisa kuhusu matarajio ya siku za zao za usoni. Ni katika wakati huu tu ndipo usafishaji wa Mungu utafikia kikomo. Mwanadamu bado hajafikia hatua ya kuelea kati ya maisha na kifo, na hajaonja mauti, hivyo mchakato wa usafishaji bado haujakamilika. Hata wale ambao walikuwa katika hatua ya watenda huduma hawakuwa wamesafishwa kabisa. Ayubu alipitia usafishaji mkali sana, na hakuwa na kitu cha kutegemea. Watu lazima wapitie usafishaji mpaka ile hatua ambayo hawana matumaini na kitu cha kutegemea—huu tu ndio usafishaji wa kweli. Unapitia majaribu ya Ayubu, na wakati uo huo unapitiaa majaribu ya Petro. Wakati Ayubu alijaribiwa, yeye alikuwa shahidi, na mwishowe, Yehova alidhihirishwa kwake. Ni baada tu ya kuwa shahidi ndipo alistahili kuona uso wa Mungu.

2 Kwa nini inasemwa: “Mimi najificha kutoka nchi ya uchafu lakini Najionyesha kwa ufalme mtakatifu”? Hiyo ina maana kwamba wakati tu uko mtakatifu na kuwa shahidi ndipo unaweza kuwa na hadhi ya kuuona uso wa Mungu. Kama huwezi kuwa shahidi kwa ajili Yake, hauna hadhi ya kuuona uso Wake. Ukijiondoa au kufanya malalamiko kwa Mungu ukikabiliwa na usafishaji, hivyo ushindwe kuwa shahidi Wake na uwe kichekesho cha Shetani, basi hutapata sura ya Mungu. Kama wewe ni kama Ayubu, ambaye katikati ya majaribu aliulaani mwili wake na wala hakulalamika dhidi ya Mungu, na aliweza kuuchukia mwili wake bila kulalamika au kutenda dhambi kwa njia ya maneno yake, basi utakuwa shahidi. Unapopitia usafishaji kwa kiasi fulani na bado unaweza kuwa kama Ayubu, mtiifu kabisa mbele ya Mungu na bila mahitaji mengine Kwake au dhana zako mwenyewe, basi Mungu atakuonekania.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaopaswa Kukamilishwa Lazima Wapitie Usafishaji” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 672 Majaribio ya Mungu kwa Wanadamu ni ili Kuwatakasa

Inayofuata: 674 Yote Afanyayo Mungu ni Kumkamilisha na Kumpenda Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp