585 Stahimili Mzigo Zaidi ili Ukamilishwe kwa Urahisi Zaidi na Mungu

1 Kadiri unavyozingatia mapenzi ya Mungu, ndivyo unavyokuwa na mzigo zaidi; kadiri unavyokuwa na mzigo, ndivyo uzoefu wako utakuwa mwingi zaidi. Unapokuwa mzingatifu wa mapenzi ya Mungu, Mungu atakupa mzigo huu, na Mungu atakupa nuru ya mambo ambayo amekuaminia. Baada ya Mungu kukupa mzigo huu, utaangalia ukweli wa kipengele hiki unapokula na kunywa maneno ya Mungu.

2 Kama una mzigo unaohusiana na hali ya maisha ya ndugu, huu ni mzigo ulioaminiwa kwako na Mungu, na sala zako za kila siku daima zitaubeba mzigo huu. Kile ambacho Mungu hufanya kimeaminiwa kwako, uko radhi kutekeleza kile ambacho Mungu anataka kufanya, na hivi ndivyo inavyomaanisha kuuchukua mzigo wa Mungu kama wako.

3 Unapokuwa ukila na kunywa maneno ya Mungu na wakati huo kuubeba mzigo, unakuwa na uwezo wa kuelewa kiini cha maneno ya Mungu, kutafuta njia yako, na kuzingatia mapenzi ya Mungu. Kwa hivyo, unapaswa kumsihi Mungu akuongezee mizigo zaidi katika sala zako ili aweze kukuaminia mambo makuu zaidi, unaweza vyema zaidi kupata njia ya utendaji mbele, unakuwa wa kufaa zaidi katika kula na kunywa maneno ya Mungu, unakuwa na uwezo wa kuelewa kiini cha maneno Yake, na unaweza zaidi kukubali kuguswa hisi na Roho Mtakatifu. Kula na kunywa maneno ya Mungu, kufanya maombi, kukubali mzigo wa Mungu, kukubali Anachokuaminia—haya yote ni kwa ajili ya kuwa na njia mbele yako. Kadiri unavyozidi kuwa na mzigo mwingi wa agizo la Mungu, ndivyo itakavyokuwa rahisi zaidi kwako kufanywa mtimilifu na Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Kuwa Mzingatifu wa Mapenzi ya Mungu ili Upate Utimilifu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 584 Jitoe Kikamilifu Kwa Kazi ya Mungu

Inayofuata: 586 Poteza Nafasi na Utajuta Milele

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp