496 Tenda Ukweli Zaidi ili Kuendelea Zaidi Maishani

1 Ukweli ambao mwanadamu anahitaji kuwa nao unapatikana katika neno la Mungu, na ni ukweli wenye manufaa na usaidizi zaidi kwa wanadamu. Ni dawa na ruzuku ambayo miili yenu inahitaji, kitu kinachomsaidia mwanadamu kurejesha tena ubinadamu wake wa kawaida. Ni ukweli ambao mwanadamu anapaswa kujitayarisha nao. Kadiri mnavyotenda neno la Mungu, ndivyo maisha yenu yatakavyositawi haraka zaidi, na ndivyo ukweli utakavyokuwa dhahiri zaidi. Mnapozidi kukua katika kimo, mtaona vitu vya dunia ya kiroho kwa dhahiri zaidi, na ndivyo mtakavyokuwa na nguvu zaidi kumshinda Shetani. Ukweli mwingi ambao hamwelewi utafanywa kuwa dhahiri mtakapotenda neno la Mungu.

2 Watu wengi wanaridhishwa kuelewa tu maandiko ya neno la Mungu na hawalengi kujitayarisha kwa mafundisho badala ya kuzidisha uzoefu wao kwa vitendo, lakini, je, hiyo si njia ya Mafarisayo? Kwa hivyo msemo “Neno la Mungu ni uzima” unawezaje kuwa wa kweli kwao? Maisha ya mtu hayawezi kukua kwa kusoma neno la Mungu tu, bali ni wakati tu neno la Mungu linawekwa katika vitendo. Ikiwa unaamini kwamba kuelewa neno la Mungu ndicho kitu pekee kinachohitajika kuwa na uzima na kimo, basi ufahamu wako umepotoka. Kuelewa neno la Mungu kwa kweli hutokea unapoweka ukweli katika vitendo, na ni lazima uelewe kwamba “ni kwa kutenda ukweli tu ndipo unaweza kueleweka.”

Umetoholewa kutoka katika “Punde Unapoelewa Ukweli, Unapaswa Kuuweka Katika Vitendo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 495 Tenda Ukweli Kwa Ajili ya Badiliko la Kweli

Inayofuata: 497 Kutenda Ukweli Kunahitaji Gharama ya Kweli

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp