772 Kadri Unavyozidi kumridhisha Mungu, Ndivyo Unavyozidi Kubarikiwa

1 Kadri unavyomridhisha Mungu, ndivyo Mungu hukubariki zaidi, na ndivyo nguvu za upendo wako kwa Mungu huwa kuu zaidi; kwa hiyo, vilevile, utakuwa na imani na azimio, na utahisi kwamba hakuna kilicho na thamani zaidi au cha maana kuliko kutumia maisha ukimpenda Mungu. Inaweza kusemwa kwamba mwanadamu anatakiwa tu kumpenda Mungu ili kuishi bila huzuni. Ingawa kuna nyakati ambazo mwili wako ni dhaifu na unazongwa na matatizo mengi ya kweli, katika nyakati hizi utamtegemea Mungu kweli, na ndani ya roho yako utafarijiwa, na utahisi hakika, na kwamba una kitu cha kutegemea. Kwa njia hii, utaweza kushinda hali nyingi, na kwa hiyo hutalalamika kuhusu Mungu kwa sababu ya uchungu unaopitia; utataka kuimba, kucheza, na kuomba, kukusanyika na kuwasiliana kwa karibu, kumfikiria Mungu, na utahisi kwamba watu wote, mambo, na vitu vilivyo kandokando yako ambavyo vimepangwa na Mungu vinafaa.

2 Kadri unavyomridhisha Mungu, ndivyo Mungu hukubariki zaidi, na ndivyo nguvu za upendo wako kwa Mungu huwa kuu zaidi; kwa hiyo, vilevile, utakuwa na imani na azimio, na utahisi kwamba hakuna kilicho na thamani zaidi au cha maana kuliko kutumia maisha ukimpenda Mungu. Kama humpendi Mungu, yote ambayo unategemea yatakuwa yenye kero kwako, hakuna kitakachokuwa cha kufurahisha machoni mwako; ndani ya roho yako hutakuwa huru bali wa kudhulumiwa, moyo wako daima utalalamika kuhusu Mungu, na daima utahisi kwamba unapitia mateso mengi sana, na kwamba ni udhalimu sana. Kama hufuatilii kwa ajili ya furaha, bali ili umridhishe Mungu na kutoshtakiwa na Shetani, basi ukimbizaji kama huo utakupa nguvu nyingi za kumpenda Mungu. Mwanadamu anaweza kutekeleza yote yanayonenwa na Mungu, na yote ayafanyayo yanaweza kumridhisha Mungu—hii ndiyo maana ya kuwa na hakika.

Umetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 771 Mungu Awalinda Wale Wampendao

Inayofuata: 773 Uko Tayari Kumpa Mungu Upendo Ulio Moyoni Mwako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp