37 Kusonga kwa Kazi ya Mungu Ulimwenguni

1 Nimepita kati ya wanadamu kwa miaka mingi, lakini hajawahi kufahamu hili, na hajawahi kunijua. Leo Namwambia hili kwa kinywa Changu mwenyewe, na kufanya watu wote waje mbele Yangu kupata kitu kutoka Kwangu, lakini bado wanaendelea kukaa mbali Nami, na hivyo basi hawanijui. Wakati nyayo Zangu zitaukanyaga ulimwengu mzima na hadi miisho ya dunia, mwanadamu ataanza kutafakari juu yake mwenyewe, na watu wote watakuja Kwangu na kusujudu mbele Zangu na kuniabudu. Hii itakuwa siku ya utukufu Wangu, siku ya kurudi Kwangu, na pia siku ya kuondoka Kwangu.

2 Sasa, Nimeanza Kazi Yangu miongoni mwa watu wote, Nimeanza kirasmi, katika ulimwengu wote, ukamilishaji wa mpango Wangu wa usimamizi. Kuanzia sasa na kuendelea, wowote ambao si waangalifu wanastahili kutumbukizwa katikati ya kuadibu kusiko na huruma wakati wowote. Hii si kwa sababu Mimi sina utu, lakini ni hatua ya mpango Wangu wa usimamizi; zote lazima ziendelee kulingana na hatua za Mpango Wangu, na hakuna mwanadamu anayeweza kubadili hali hii.

3 Ninapoanza kirasmi Kazi Yangu, watu wote wanatembea kama Mimi hatua kwa hatua, kiasi kwamba watu katika ulimwengu wote wanakuwa katika hatua na Mimi, kuna “shangwe” ulimwengu mzima, na mwanadamu anaendelezwa mbele na Mimi. Kwa sababu hii, joka kubwa jekundu mwenyewe anachapwa na Mimi mpaka anakuwa katika hali ya kuchanganyikiwa na wazimu, na anahudumia Kazi Yangu, na, licha ya kutokuwa na nia, anashindwa kufuata tamaa zake mwenyewe, na kukosa njia nyingine ila kujiwasilisha kwa udhibiti Wangu.

4 Katika mipango Yangu yote, joka kubwa jekundu ni foili Yangu, adui Wangu, na pia mtumishi Wangu; kwa hivyo, Sijawahi kushusha “mahitaji” Yangu kwake. Kwa hivyo, hatua ya mwisho ya kazi Yangu katika mwili inakamilika katika nyumba ya joka huyu. Kwa njia hii, joka kubwa jekundu anapata uwezo zaidi wa kunitumikia Mimi vizuri, kwa njia ambayo Mimi Nitamshinda na kukamilisha Mpango Wangu. Ninapofanya kazi, malaika wote wanaanzisha vita vya maamuzi na Mimi na kuamua kutimiza matakwa Yangu katika hatua ya mwisho, ili watu walio duniani wajitoe Kwangu kama malaika, na wasiwe na haja ya kunipinga Mimi, na wasifanye chochote ambacho kinaniasi. Hii ndio elimumwendo ya kazi Yangu kotekote katika ulimwengu.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 29” ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 36 Mungu Amefanya Kazi Mpya Katika Ulimwengu Mzima

Inayofuata: 38 Mungu Mwenyewe Akujapo Duniani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp