177 Umuhimu wa Kupata Mwili kwa Mungu

1 Mwili wa mwanadamu umepotoshwa na Shetani, na wengi wamepofushwa, na kuumizwa sana. Sababu muhimu sana ambayo inamfanya Mungu kufanya kazi katika mwili ni kwa sababu mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, ambaye ni wa mwili, na kwa sababu Shetani pia anatumia mwili wa mwanadamu kusumbua kazi ya Mungu. Vita na Shetani kwa hakika ni kazi ya kumshinda mwanadamu, na wakati uo huo mwanadamu pia ni mlengwa wa wokovu wa Mungu. Kwa njia hii, kazi ya Mungu mwenye mwili ni muhimu.

2 Shetani aliupotosha mwili wa mwanadamu, na mwanadamu akawa mfano halisi wa Shetani, na akawa mlengwa wa kushindwa na Mungu. Kwa njia hii, kazi ya kupambana na Shetani na kumwokoa mwanadamu inatokea duniani, na Mungu ni lazima awe mwanadamu ili aweze kupambana na mwanadamu. Hii ni kazi yenye utendaji wa hali ya juu.

3 Mungu anapofanya kazi katika mwili, kwa hakika Anapambana na Shetani katika mwili. Anapofanya kazi katika mwili, Anafanya kazi Yake katika ulimwengu wa kiroho, na Anafanya kazi Yake yote katika ufalme wa kiroho ili iwe halisi duniani. Anayeshindaniwa ni mwanadamu, asiye mtiifu Kwake, yule anayeshindwa ni mfano halisi wa Shetani, ambaye ana uadui na Yeye, na ambaye ataokolewa hatimaye ni mwanadamu. Kwa namna hii, ni muhimu zaidi Kwake kuwa mwanadamu ambaye ana ganda la nje la kiumbe, ili kwamba Awe na uwezo wa kupambana na Shetani katika uhalisi, kumshinda mwanadamu, ambaye si mtiifu Kwake na ambaye ana kuonekana kwa nje ambako kunafanana na Yeye, na kumwokoa mwanadamu, ambaye ana umbo la nje kama Lake na aliyeumizwa na Shetani.

4 Adui Wake ni mwanadamu, mlengwa wa ushindi Wake ni mwanadamu, na mlengwa wa wokovu Wake ni mwanadamu, aliyeumbwa na Yeye. Hivyo ni lazima Awe mwanadamu, na kwa njia hii, kazi Yake inakuwa rahisi zaidi. Ana uwezo wa kumshinda Shetani na kumshinda mwanadamu, aidha, anaweza kumwokoa mwanadamu.

Umetoholewa kutoka katika “Mwanadamu Aliyepotoka Anahitaji Zaidi Wokovu wa Mungu Mwenye Mwili” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 176 Mungu Alikuwa Mwili Kufanya Kazi kwa Ajili ya Mwanadamu

Inayofuata: 178 Mungu Mwenye Mwili Afanya Kazi Muhimu Zaidi ya Kumwokoa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp