975 Amri za Enzi Mpya Ni Muhimu Sana

1 Maana ya amri za enzi mpya ni kubwa sana. Zinaonyesha kwamba Mungu kweli ataonekana kwenye ardhi naye Mungu ataushinda ulimwengu mzima juu ya nchi, akiuonyesha utukufu Wake wote katika mwili. Pia zinaonyesha kwamba Mungu wa vitendo anaenda kuifanya kazi zaidi ya vitendo duniani ili akamilishe yote ambayo Amechagua. Zaidi ya hayo, Mungu atatimiza kila kitu kwa maneno duniani na kufanya wazi amri kwamba “Mungu mwenye mwili huinuka juu zaidi naye ametukuzwa, nao watu wote na mataifa yote hupiga magoti kumwabudu Mungu—ambaye ni mkuu.” Ingawa amri za enzi mpya ni za mwanadamu kuzishika, na ingawa kufanya hivyo ni wajibu wa mwanadamu na jukumu lake, maana ambazo zinawakilisha ni ya kina sana kuweza kuonyeshwa kikamilifu katika neno moja au mawili. Amri za enzi mpya zinachukua nafasi ya sheria za Agano la Kale na maagizo ya Agano Jipya kama zilivyotangazwa rasmi na Yehova na Yesu. Hili ni somo la ndani zaidi, sio jambo rahisi kama mtu anavyoweza kufikiria.

2 Amri za enzi mpya zinazo kipengele cha maana ya vitendo: Zinatumika kama kipengee kinachojitokeza kati ya Enzi ya Neema na Enzi ya Ufalme. Amri za enzi mpya zinahitimisha mazoea yote na maagizo yote ya enzi ya zamani na pia zinahitimisha mazoea yote ya enzi ya Yesu na zile kabla yake. Zinamleta mwanadamu katika uwepo wa Mungu wa vitendo zaidi na kumruhusu mtu kuanza kuupokea ukamilifu wa binafsi wa Mungu, ambazo ni mwanzo wa njia ya kukamilika. Kwa hiyo, ninyi mtamiliki mtazamo sahihi kuelekea amri za enzi mpya na wala hamtazifuata ovyo wala kuzidharau. Amri za enzi mpya zinasisitiza hoja moja: kwamba mwanadamu atamwabudu Mungu wa vitendo Mwenyewe wa leo, ambayo ni kutii kiini cha Roho katika matendo zaidi. Pia zinasisitiza kanuni ambayo Mungu atamhukumu mwanadamu kuwa na hatia au haki Atakapoonekana kama Jua la haki.

Amri za enzi mpya zinaashiria kuwa Mungu na binadamu wameingia katika eneo la mbingu mpya na nchi mpya, na kwamba Mungu, kama vile Yehova alifanya kazi miongoni mwa Waisraeli naye Yesu alifanya kazi miongoni mwa Wayahudi, Ataifanya kazi zaidi ya vitendo na kuifanya kazi zaidi na kubwa zaidi duniani.

Umetoholewa kutoka katika “Kuzishika Amri na Kuutenda Ukweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 974 Amri za Enzi Mpya

Inayofuata: 976 Yatii Mapenzi ya Mungu kwa Kufuata Amri Kumi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp