Sura ya 96

Nitamwadibu kila mtu aliyezaliwa kutoka Kwangu ambaye bado hanijui ili kuonyesha ghadhabu Yangu yote, kuonyesha nguvu Zangu kuu, na kuonyesha hekima Yangu kamili. Ndani Yangu kila kitu ni chenye haki na bila shaka hakuna udhalimu, hakuna udanganyifu, na hakuna upotovu; yeyote ambaye ni mpotovu na mdanganyifu lazima awe ni mwana wa jahanamu—lazima amezaliwa huko kuzimu. Ndani Yangu kila kitu ni cha wazi; chochote Ninachosema kukamilisha kinakamilika na chochote Ninachosema kuanzisha kinaanzishwa, na hakuna mtu anayeweza kubadilisha au kuiga mambo haya kwa sababu Mimi ndimi Mungu Mwenyewe wa pekee. Katika kinachokaribia kuja, kila mtu aliye katika kikundi cha wazaliwa Wangu wa kwanza walioamuliwa kabla na walioteuliwa watafichuliwa mmoja baada ya mwingine, na yeyote asiye katika kikundi cha wazaliwa wa kwanza ataondolewa na Mimi kupitia kwa hili. Hivi ndivyo Ninavyofanya na kukamilisha kazi Yangu. Hivi sasa, Ninawafunua watu wengine ili tu kwamba wazaliwa Wangu wa kwanza waweze kuona matendo Yangu ya ajabu, lakini baadaye Sitafanya kazi kwa njia hii. Badala yake, Nitaendelea kutoka kwa hali ya kawaida badala ya kuwaacha waonyeshe hali zao za kweli mmoja baada ya mwingine (kwa sababu kimsingi mapepo wote ni sawa, inatosha tu kuchagua wachache kama vithibitisho). Wazaliwa Wangu wa kwanza wote wanaelewa vyema, na hakuna haja ya Mimi kufafanua (kwa sababu katika wakati uliowekwa, hakika wao watafichuliwa mmoja baada ya mwingine).

Ni tabia Yangu kutimiza ahadi Zangu, na ndani Yangu hakuna kitu kilichofichwa au kilichofichika. Nitawaambia kila kitu kuhusu kila mojawapo ya vitu ambavyo mnapaswa kuelewa, na Sitawaambia kabisa kuhusu kitu chochote msichopaswa kujua, msije mkakosa kusimama imara. Msishikilie vitu vidogo vidogo na hapo mpoteze mambo muhimu—hakika hiyo haina thamani kabisa. Amini kwamba Mimi ni mwenyezi Mungu na kila kitu kitafanikishwa na vyote vitakuwa rahisi na vya kupendeza. Hivi ndivyo Ninavyofanya mambo. Yeyote anayeamini, Ninamruhusu aone, na yeyote asiyeamini, Simruhusu kujua na Simruhusu aelewe kamwe. Ndani Yangu hakuna hisia au rehema, na yeyote anayekosea kuadibu Kwangu hakika Nitamuua bila kumhurumia, Nikiwatendea wote sawa. Mimi niko sawa kwa kila mtu—Sina hisia za kibinafsi nami Sitendi kwa kuonyesha hisia hata kidogo. Je, watu wanawezaje kukosa kuona haki na uadhama Wangu kupitia katika hili? Hii ni hekima Yangu na tabia Yangu, ambayo hakuna mtu anayeweza kubadilisha na hakuna mtu anayeweza kujua kabisa. Daima mikono Yangu inadhibiti kila kitu, wakati wote, na Mimi hupanga kila kitu kunihudumia kwa amri Yangu wakati wowote. Watu wengi wanatoa huduma kwa niaba Yangu ili kutimiza mpango Wangu wa usimamizi, lakini hatimaye wanaziona baraka lakini hawawezi kuzifurahia—ni ya kusikitisha jinsi gani! Lakini hakuna mtu anayeweza kuubadilisha moyo Wangu. Hii ni amri Yangu ya utawala (inapokuja kwa amri ya utawala, hiyo ndiyo hakuna mtu anayeweza kubadilisha, hivyo Ninapozungumzia wakati ujao, kama Nimepania kitu, hakika hiyo ni amri Yangu ya utawala. Kumbuka! Usifanye makosa dhidi ya hili, usije ukapoteza), na pia ni sehemu ya mpango Wangu wa usimamizi. Ni kazi Yangu mwenyewe, si kitu tu ambacho mtu yeyote anaweza kufanya. Lazima Nifanye jambo hili—ni lazima Nipange hili, ambayo inatosha kuonyesha kudura Yangu na kudhihirisha ghadhabu Yangu.

Watu wengi bado hawajui na hawaelewi kuhusu ubinadamu Wangu. Nimesema mara kadhaa, lakini ninyi bado hamna uhakika na hamwelewi sana. Lakini hii ni kazi Yangu, na sasa, wakati huu, yeyote anayejua, anajua, na yeyote asiyejua, Simshawishi. Inaweza tu kuwa namna hii. Nimezungumza waziwazi na Sitasema baadaye (kwa sababu Nimesema mengi sana, na Nimeyasema wazi sana. Mtu ambaye ananijua hakika ana kazi ya Roho Mtakatifu na bila shaka ni mmoja wa wazaliwa Wangu wa kwanza. Mtu ambaye hanijui amefanya uamuzi kutonijua, ikithibitisha kwamba Nimeshaondoa Roho Wangu kutoka kwake). Lakini mwishowe, Nitamfanya kila mtu anijue—anijue kabisa katika ubinadamu Wangu na katika utakatifu Wangu. Hizi ni hatua za kazi Yangu, na lazima Nifanye kazi kwa njia hii. Hii pia ni amri Yangu ya utawala. Lazima kila mtu aniite Mimi Mungu pekee wa kweli, na kunisifu na kunihimidi bila kukoma.

Mpango Wangu wa usimamizi umekwisha kukamilishwa kabisa, na kila kitu kimefanikishwa kitambo. Kwa macho ya binadamu inaonekana kana kwamba kazi Yangu nyingi bado inaendelea, lakini tayari Nimeipanga vizuri na yote ambayo yanatarajiwa ni ukamilisho wake kwa kulingana na hatua Zangu kazi moja baada ya nyingine (hii ni kwa sababu kabla ya uumbaji wa ulimwengu Nilishajaalia ni nani anaweza kusimama imara katika majaribu, nani hawezi kuteuliwa na kuamuliwa kabla na Mimi, na nani hawezi kushiriki katika mateso Yangu. Wale ambao wanaweza kushiriki katika mateso Yangu—yaani, wale walioamuliwa kabla na kuteuliwa na Mimi, hakika Nitawahifadhi na kuwawezesha kuvuka mipaka ya kila kitu). Niko dhahiri moyoni Mwangu kuhusu nani aliye katika kila jukumu. Najua vema ni nani anayetoa huduma Kwangu, ni nani mzaliwa wa kwanza, na ni nani aliye kati ya wana Wangu na watu Wangu. Najua jambo hili kama kiganja cha mkono Wangu. Mtu yeyote Niliyesema zamani kuwa ni mzaliwa wa kwanza bado ni mzaliwa wa kwanza sasa, na yeyote Niliyesema zamani kuwa si mzaliwa wa kwanza bado si mzaliwa wa kwanza sasa. Chochote Ninachokifanya, Sijuti, na Sikibadilishi kwa urahisi. Namaanisha kile Ninachosema (ndani Yangu hakuna chochote kisicho na maana), na hakibadiliki kamwe! Wale ambao wanatoa huduma Kwangu daima hutoa huduma Kwangu: Wao ni ng'ombe Wangu; wao ni farasi Wangu (lakini watu hawa hawajawahi kupata nuru katika roho zao, Ninapowatumia wao huwa muhimu, lakini wakati Siwatumii Ninawaua. Ninapozungumza kuhusu ng'ombe na farasi, Ninamaanisha wale ambao hawajapata nuru katika roho zao, ambao hawanijui, na ambao wananiasi, na hata kama wao ni watiifu na wanyenyekevu na wepesi na waaminifu, wao bado ni ng'ombe na farasi halisi). Sasa, watu wengi ni watukutu na hawajafunguliwa mbele Yangu, wakiongea na kucheka kwa fujo, wakitenda kwa namna isiyo ya heshima—wanaona tu ubinadamu Wangu, na sio uungu Wangu. Katika ubinadamu Wangu tabia hizi zinaweza kukubaliwa bila lawama na Niweze kuzisamehe, lakini katika uungu Wangu si rahisi sana. Katika siku zijazo Nitaamua kwamba wewe umetenda dhambi kwa kunikufuru. Kwa maneno mengine, ubinadamu Wangu unaweza kukosewa, lakini uungu Wangu hauwezi, na yeyote anayepingana na Mimi kidogo, Nitamhukumu mara moja, bila kuchelewa. Usifikiri kuwa kwa sababu umeshirikiana kwa miaka mingi na mtu huyu Niliye na umejuana na Mimi, unaweza kuzungumza na kutenda kwa utukutu. Kwa kweli Sijali sana! Haijalishi ni nani, Nitamtendea kwa haki. Hii ni haki Yangu.

Siri Zangu zinafichuliwa kwa watu kila siku, nazo huwa wazi zaidi kila siku, zikifuata hatua za ufunuo, ambayo inatosha kuonyesha kasi ya kazi Yangu. Hii ni hekima Yangu (Siisemi moja kwa moja. Ninawapa nuru wazaliwa Wangu wa kwanza na kuwapofusha watoto wa joka kuu jekundu). Zaidi ya hayo, leo Nitawafichulia siri Yangu kupitia kwa mwanangu. Mambo ambayo hayafikiriki na watu Nitawafichulia leo ili kuwawezesha kujua kabisa na muwe na ufahamu dhahiri. Zaidi ya hayo, siri hii ipo ndani ya kila mtu nje ya wazaliwa Wangu wa kwanza, lakini hakuna mtu anayeweza kuielewa. Ingawa imo ndani ya kila mtu, hakuna mtu anayeweza kuitambua. Ninasema nini? Katika kazi Yangu wakati huu na katika matamshi Yangu wakati huu, mara nyingi Mimi hutaja joka kuu jekundu, Shetani, ibilisi, na malaika mkuu. Wao ni nini? Je, uhusiano wao ni nini? Ni nini kinachojidhihirisha katika mambo haya? Udhihirisho wa joka kuu jekundu ni upinzani Kwangu, ukosefu wa ufahamu na utambuzi wa maana ya maneno Yangu, mateso ya mara kwa mara Kwangu, na kutafuta kutumia njama ili kuzuia usimamizi Wangu. Shetani anadhihirika kama ifuatavyo: kupambania mamlaka na Mimi, kutaka kuwamiliki watu Wangu wateule, na kutoa maneno hasi ili kuwadanganya watu Wangu. Udhihirisho wa ibilisi (wale ambao hawalikubali jina Langu, ambao hawaamini, wote ni mapepo) ni kama ifuatavyo: kupenda raha za mwili, kujiingiza katika tamaa mbaya, kuishi chini ya utumwa wa Shetani, wengine kupinga na wengine kuniunga mkono (lakini kutothibitisha kwamba wao ni wana Wangu wapendwa). Udhihirisho wa malaika mkuu ni kama ifuatavyo: kuzungumza kwa kiburi, kuwa asiyemcha Mungu, mara nyingi kuchukua sauti Yangu kuwahubiria watu, kuzingatia tu kuniiga kwa nje, kula kile Ninachokula na kutumia kile Ninachotumia; kwa ufupi, kutaka kuwa sawa na Mimi, kuwa mwenye tamaa ya makuu lakini kukosa ubora Wangu na kutokuwa na maisha Yangu, kuwa bure. Shetani, ibilisi, na malaika mkuu ni maonyesho ya mfano hasa wa joka kuu jekundu, kwa hiyo wale ambao hawajaamuliwa kabla na kuchaguliwa na Mimi wote ni watoto wa joka kuu jekundu: Hiyo ni hivyo kabisa! Hawa wote ni adui Zangu. (Hata hivyo mivurugo ya Shetani haihusishwi. Ikiwa asili yako ni ubora Wangu, hakuna mtu anayeweza kuibadilisha. Kwa sababu sasa bado unaishi katika mwili, mara kwa mara utakabiliwa na majaribu ya Shetani—hii haiwezi kuepukika—lakini lazima daima uwe makini.) Kwa hiyo, Nitawaacha watoto wote wa joka kuu jekundu nje ya wazaliwa Wangu wa kwanza. Asili yao haiwezi kubadilika daima, nao ni ubora wa Shetani. Ni ibilisi wanayemdhihirisha, na ni malaika mkuu wanayeishi kwa kumdhihirisha. Hii ni kweli kabisa. Joka kuu jekundu Ninayezungumzia si joka kuu jekundu lolote fulani; badala yake ni pepo mbaya anayenipinga Mimi, ambaye kwaye “joka kuu jekundu” ni kisawe. Hivyo roho zote nje ya Roho Mtakatifu ni roho mbaya, na zinaweza pia kusemwa kuwa ni watoto wa joka kuu jekundu. Haya yote yanapaswa kuwa wazi kabisa kwa kila mtu.

Iliyotangulia: Sura ya 95

Inayofuata: Sura ya 97

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp