922 Hakuna Mtu ama Kitu Kinachoweza Kuzidi Mamlaka na Nguvu ya Mungu
1 Ingawa Shetani alimwangalia Ayubu kwa macho ya kutamani mali yake, bila ya ruhusa ya Mungu hakuthubutu kugusa hata unywele mmoja wa mwili wa Ayubu. Ingawa ni mwenye uovu na unyama wa ndani, baada ya Mungu kutoa shurutisho Lake kwake, Shetani hakuwa na chaguo lakini kutii shurutisho la Mungu. Tunaona kwamba Shetani hathubutu kuvunja matamshi yoyote yale ya Yehova Mungu. Kwake Shetani, kila neno kutoka kwenye kinywa cha Mungu ni shurutisho, na sheria ya mbinguni, na maonyesho ya mamlaka ya Mungu—kwani nyuma ya kila neno la Mungu kunadokezwa adhabu ya Mungu kwa wale wanaokiuka maagizo ya Mungu, na wale wasiotii na wanaopinga sheria za mbinguni.
2 Vitendo vya Shetani kwake Ayubu vilikuwa tu mfano mdogo wa yeye kumpotosha binadamu, na wakati ambapo Shetani alipokuwa akitekeleza vitendo hivi, ile mipaka ambayo Mungu Aliweka na amri Alizotoa kwake Shetani vilikuwa tu mfano mdogo wa kanuni zinazotokana na kila kitu anachofanya. Aidha, wajibu na nafasi ya Shetani katika suala hili ulikuwa tu mfano mdogo wa wajibu na nafasi yake katika kazi ya usimamizi wa Mungu, na utiifu kamili wa Shetani kwa Mungu wakati alipomjaribu Ayubu, ulikuwa tu mfano mdogo wa namna ambavyo Shetani hakuthubutu kuweka hata upinzani mdogo kwa Mungu katika kazi ya usimamizi wa Mungu.
3 Miongoni mwa mambo yote, akiwemo Shetani, hakuna mtu au kitu kinachoweza kukiuka sheria na kanuni za mbinguni zilizowekwa wazi na Muumba, na hakuna mtu au kitu kinachothubutu kukiuka sheria na kanuni hizi za mbinguni, kwani hakuna mtu au kifaa kinaweza kubadilisha au kuepuka adhabu ambayo Mungu anawawekea wale wanaokosa kumtii. Ni Muumba tu anayeweza kuanzisha sheria na kanuni za mbinguni, ni Muumba tu aliye na nguvu za kuanza kuzitekeleza na nguvu za Muumba ndizo haziwezi kukiukwa na mtu au kitu chochote. Haya ndiyo mamlaka ya kipekee ya Muumba, mamlaka haya yako juu zaidi miongoni mwa mambo yote, na kwa hivyo haiwezekani kusema kwamba “Mungu ndiye mkubwa zaidi naye Shetani ni nambari mbili.” Isipokuwa Muumba anayemiliki mamlaka ya kipekee, hakuna Mungu mwingine.
Umetoholewa kutoka katika “Mungu Mwenyewe, Yule wa Kipekee I” katika Neno Laonekana katika Mwili