259 Hakuna Anayeelewa Matamanio ya Mungu Yenye Bidii ya Kumwokoa Mwanadamu

1 Mungu aliumba dunia hii na kuleta mwanadamu, kiumbe hai ambaye alitia uhai ndani yake. Kisha, mwanadamu akaja kuwa na wazazi na jamaa na hakuwa mpweke tena. Tangu mwanadamu alipotua macho kwa mara ya kwanza katika dunia hii ya mali, ilibainika kuwa angeishi ndani ya utaratibu wa Mungu. Ni pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ndiyo hustawisha kila kiumbe hai katika ukuaji wake hadi kinapokomaa. Wakati wa mchakato huu, hakuna anayehisi kwamba mwanadamu anakua chini ya uangalizi wa Mungu, bali badala yake anaamini kwamba mwanadamu anafanya hivyo chini ya utunzaji wa upendo wa wazazi wake, na kwamba ni silika yake mwenyewe ya maisha ambayo inaongoza mchakato huu wa kukua kwake. Hii ni kwa sababu mwanadamu hajui aliyeleta maisha au yalikotoka maisha hayo, sembuse jinsi silika ya maisha husababisha miujiza.

2 Anajua tu kwamba chakula ndicho msingi wa kuendelea kwa maisha yake, kwamba uvumilivu ndio chanzo cha kuwepo kwake, na kwamba imani zilizomo akilini mwake ndizo raslimali ambazo kwazo kuendelea kuishi kwake kunategemea. Mwanadamu hajui kabisa kuhusu neema na riziki zitokazo kwa Mungu, na kwa njia hii yeye hupoteza. uzima aliopewa na Mungu bila azma…. Hakuna hata mmoja wa wanadamu hawa ambaye Mungu anamwangazia usiku na mchana huchukua jukumu la kumwabudu. Mungu anaendelea tu kufanya kazi juu ya mwanadamu, akiwa hana matarajio yoyote kutoka kwake, kama jinsi ambavyo Amepanga. Anafanya hivyo kwa matumaini kwamba siku moja, mwanadamu ataamka kutoka katika ndoto yake na ghafla kuelewa thamani na maana ya maisha, gharama aliyolipa Mungu kwa yote ambayo Amempa, na wasiwasi wa hamu ambao kwao Mungu anangoja mwanadamu amgeukie.

Umetoholewa kutoka katika “Mungu Ndiye Chanzo cha Uhai wa Mwanadamu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 258 Mfano Halisi wa Nguvu Uzima ya Mungu

Inayofuata: 260 Kwa Ajili ya Uzima wa Mwanadamu, Mungu Anastahimili Mateso Yote

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp