259 Hakuna Majuto wala Malalamiko katika Kumpenda Mungu

1 Ee Mungu! Nina bahati sana kukutana nawe katika maisha haya na kukubali maneno Yako kama uzima wangu. Kila kitu Unachosema, kila tamko Utoalo linaugusa moyo wangu. Ni Wewe tu Unayeyajali maisha yangu, Ulichosema kimenifanya nielewe ukweli. Maneno Yako yananihukumu na kufunua upotovu na uasi wangu, nimeshawishika kabisa na naanguka chini mbele Yako. Kupitia majaribu Unafunua na kutakasa tabia yangu potovu, naelewa dhamira Yako ya dhati. Pia Unanipogoa na kushughulikia nia yangu ya kupata baraka kupitia imani; hatimaye najua jinsi ya kumwamini Mungu. Nimepata mengi sana kupitia maneno Yako, nikipitia kazi Yako nimefanikisha mabadiliko. Niko tayari kutoa kila kitu na kujitumia kwa ajili Yako, ili kutekeleza wajibu wangu wa kulipa upendo Wako.

2 Ee Mungu! Umekuja duniani, mpole na Aliyefichika, Ukionyesha maneno yanayowapa binadamu ukweli na uzima. Unakashifiwa kwa watu wa kidunia, kufuatiliwa na kuteswa na CCP, na hata malalamiko na kuelewa kwetu vibaya. Ni nani angeweza kuelewa moyo Wako kweli? Nani angeshiriki huzuni na furaha Zako? Unyanyasaji mwingi sana Umestahimili katika kimya, Ukinena na kufanya kazi bado, Ukifanya kila kitu ili kumwokoa binadamu. Upendo Wako umeuyeyusha moyo wangu usiohisi. Ninawezaje kuwa mwasi au hasi tena? Ingawa bado nina upungufu mwingi, lazima nitoe nguvu yangu yote kueneza jina Lako na kukushuhudia. Nitakupenda na kujitolea maisha yangu Kwako, nitafanya mapenzi Yako ili nikutukuze. Sitajuta au kulalamika kwa kukupenda maisha yangu yote, natamani moyo Wako upate faraja.

Iliyotangulia: 258 Uzuri wa Mungu Daima Uko Mawazoni Mwangu

Inayofuata: 260 Kumtamani Sana Mwenyezi Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

273 Upendo Safi Bila Dosari

1 Upendo ni hisia safi sana, safi bila dosari. Tumia moyo wako, tumia moyo wako kupenda na kuhisi na kutunza. Upendo hauweki masharti au...

84 Umuhumi wa Maombi

1 Maombi ni njia moja ya mwanadamu kishirikiana na Mungu, kuita Roho Wake na kuguswa na Mungu. Kadiri unavyoomba zaidi, ndivyo...

269 Nitampenda Mungu Milele

1 Ee Mungu! Maneno Yako yananiita nirudi Kwako. Nakubali kufundishwa katika ufalme Wako mchana na usiku. Mara nyingi sana nilikuwa dhaifu...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki