98 Hakuna Awezaye Kuondoka Kutoka Neno la Mungu

1 Mwelekeo wa maisha yajayo utakuwa hivi: Wale ambao watapata matamshi kutoka katika kinywa cha Mungu watakuwa na njia ya kutembea duniani, na wawe wafanya biashara au wanasayansi, au waelimishaji au wataalamu wa viwandani, wale ambao hawana maneno ya Mungu watakuwa na wakati mgumu wa kuchukua hata hatua moja, na watalazimishwa kutafuta njia ya kweli. Hiki ndicho kinamaanishwa na, “Ukiwa na ukweli utatembea ulimwengu mzima; bila ukweli, hutafika popote.” Ukweli ni huu: Mungu atatumia Njia (ikiwa na maana kwamba maneno Yake yote) kuuamuru ulimwengu wote na kumwongoza na kumshinda mwanadamu. Roho Mtakatifu anawapatia watu hisia. Baada ya kusoma maneno ya Mungu, katika mioyo yao wamesimama imara, na wana amani, wakati wale ambao hawapati maneno ya Mungu wanajihisi watupu. Hiyo ni nguvu ya maneno ya Mungu—watu wanapaswa kuyasoma, baada ya kuyasoma wananawirishwa, na hawawezi kufanya chochote bila hayo. Kusoma maneno ya Mungu kunawapatia watu nguvu. Ikiwa hawayasomi, wanajiona hawana nguvu, lakini baada ya kuyasoma, wanainuka mara moja kutoka katika “kitanda cha mgonjwa.” Hii ni neno la Mungu kutawala duniani na Mungu kutawala ulimwenguni.

2 Baadhi ya watu wanataka kuacha au wamechoshwa na kazi ya Mungu. Licha ya hayo, hawawezi kujitenganisha na maneno ya Mungu; bila kujali ni wadhaifu kiasi gani, bado ni lazima waishi kwa kutegemea maneno ya Mungu ili waishi, na haijalishi ni watu wa uasi kiasi gani, lakini bado hawathubutu kuacha maneno ya Mungu. Pale ambapo maneno ya Mungu yanaonyesha ukuu wao ndipo ambapo Mungu anatawala na kuchukua nguvu, na hivi ndivyo Mungu anavyofanya kazi. Hata hivyo, hii ndiyo njia ambayo kwayo Mungu anafanya kazi, na hakuna anayeweza kuiacha. Maneno ya Mungu yataenea katika nyumba zisizohesabika, yatafahamika kwa wote, na wakati huo tu ndipo kazi yake itaenea ulimwenguni kote. Katika siku ya utukufu wa Mungu, maneno ya Mungu yataonesha nguvu yake na mamlaka. Kila neno Lake kuanzia wakati huo hadi leo litatimizwa na kuwa la kweli. Kwa njia hii, utukufu utakuwa wa Mungu duniani—ambavyo ni sawa na kusema, kazi yake itatawala duniani.

Umetoholewa kutoka katika “Ufalme wa Milenia Umewasili” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 97 Mungu Hutumia Maneno Kuushinda Ulimwengu Mzima Katika Siku za Mwisho

Inayofuata: 99 Yote Yatimizwa Kupitia Neno la Mungu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp