354 Hakuna Ayejali Kumwelewa Mungu kwa Utendaji

1 Kila wakati Mungu anapokuwa amekasirika, Anakumbana na mwanadamu ambaye hamtilii maanani kamwe, mwanadamu anayemfuata Yeye na anayedai kumpenda Yeye lakini anapuuza kabisa hisia Zake. Moyo Wake utakosaje kuumia? Katika kazi ya usimamizi ya Mungu, Anaitekeleza kwa dhati kazi Yake na Anaongea na kila mmoja Anawatazama bila kizuizi chochote au kujificha, lakini kinyume chake ni kuwa, kila mtu anayemfuata Yeye anatenganishwa na Yeye, na hakuna aliye radhi kujishughulisha na kuwa karibu na Yeye, kuelewa moyo Wake, au kutilia maanani hisia Zake. Hata wale wanaotaka kuwa wandani wa Mungu hawataki kuwa karibu na Yeye, kutilia maanani moyo Wake, au kujaribu kumwelewa Yeye.

2 Wakati Mungu anashangilia na ana furaha, hakuna yeyote yule wa kushiriki katika furaha hiyo na Yeye. Wakati Mungu anakosa kueleweka na watu, hakuna mtu wa kutuliza moyo Wake ulio na majeraha. Wakati moyo Wake unaumia, hakuna hata mtu mmoja aliye radhi kumsikiliza Yeye na kuwa mwandani Wake. Katika hii maelfu ya miaka ya usimamizi wa kazi ya Mungu, hakuna mtu anayeelewa hisia za Mungu, hakuna hata mtu anayefahamu au kutambua hisia Zake, tupilia mbali hata yeyote ambaye angesimama kando ya Mungu ili kushiriki katika furaha na huzuni Zake. Mungu ni mpweke. Yeye ni pweke! Mungu ni mpweke si tu kwa sababu wanadamu waliopotoka wanampinga Yeye, lakini zaidi kwa sababu wale wanaofuatilia kuwa wa kiroho, wale wanaotafuta kumjua Mungu na kumwelewa Yeye, na hata wale walio radhi kujitolea maisha yao yote kwake Yeye, pia hawajui fikira Zake, na hawaielewi tabia Yake na hisia Zake.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe I” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 353 Uko Wapi Ushahidi wa Kulingana Kwako na Mungu

Inayofuata: 355 Mmempa Mungu Nini Kama Malipo?

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp