442 Ni Muhimu Kuwa na Uhusiano wa Kawaida na Mungu

1 Katika kila jambo unalofanya, sharti uchunguze ikiwa nia zako hazina makosa. Ikiwa unaweza kutenda kulingana na matakwa ya Mungu, basi uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida. Hiki ndicho kiwango cha chini kabisa. Chunguza nia zako, na ukiona kwamba nia mbaya zimejitokeza, uweze kuziacha na kutenda kulingana na maneno ya Mungu; hivyo utakuwa mtu aliye sawa mbele za Mungu, ambayo inaonyesha kwamba uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida, na kwamba yote unayoyafanya ni kwa ajili ya Mungu, si kwa ajili yako.

2 Katika yote unayofanya na yote unayosema, uweze kuuweka moyo wako uwe sawa na uwe mwenye haki katika matendo yako, na usiongozwe na hisia zako, wala kutenda kulingana na mapenzi yako mwenyewe. Hizi ni kanuni ambazowaumini katika Mungu wanapaswa kutenda. Mambo madogo yanaweza kufichua nia na kimo cha mtu, na kwa hivyo, ili mtu aweze kuingia kwenye njia ya kukamilishwa na Mungu, lazima kwanza arekebishe nia zake na uhusiano wake na Mungu.

3 Ni wakati tu uhusiano wako na Mungu unapokuwa wa kawaida ndipo unaweza kukamilishwa na Yeye; ni wakati huo tu ndipo ushughulikiaji, upogoaji, ufundishaji nidhamu, na usafishaji wa Mungu vifanikisha athari zake zilizokusudiwa ndani yako. Hiyo ni kusema, ikiwa wanadamu wanaweza kumweka Mungu mioyoni mwao na wasifuatilie faida ya kibinafsi au kufikiria matarajio yao wenyewe, lakini badala yake wabebe mzigo wa kuingia katika uzima, wajitahidi kabisa kuufuatilia ukweli, na kuitii kazi ya Mungu—ikiwa unaweza kufanya hivi, basi malengo unayoyafuatilia yatakuwa sawa, na uhusiano wako na Mungu utakuwa wa kawaida. Kama unaweza kukamilishwa na Mungu au kupatwa na Yeye kunategemea ikiwa uhusiano wako na Mungu ni wa kawaida.

Umetoholewa kutoka katika “Uhusiano Wako Na Mungu Ukoje?” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 441 Jinsi ya Kuanzisha Uhusiano wa Kawaida Na Mungu

Inayofuata: 443 Zingatia Maneno ya Mungu kwa Ajili ya Uhusiano Ufaao na Wengine

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp