411 Kumwamini Mungu Lakini Kutokubali Ukweli ni Kuwa Asiyeamini
1 Watu wengi hawapati shangwe ndani ya ukweli, na vile vile katika hukumu. Badala yake, wao hupata furaha kwa nguvu na mali; watu kama hawa wanaitwa wanaotafuta mamlaka. Wanatafuta tu madhehebu yaliyo na ushawishi duniani na wahubiri na waalimu wanaotoka katika seminari. Hata ingawa wameikubali njia ya ukweli, bado wako na shaka ndani yao na hawawezi kujitolea kikamilifu. Wanazungumzia kujinyima kwa sababu ya Mungu, lakini macho yao yamelenga tu wahubiri wakuu na waalimu, na Kristo anasukumwa pembeni. Mioyo yao imejaa umaarufu, mali na utukufu. Hawaamini kamwe kuwa mtu wa kawaida tu anaweza kuwashinda wengi vile, kwamba mtu asiye wa kutambulika kwa macho tu anaweza kukamilisha watu. Hawaamini kuwa hawa watu wasio na sifa, walio kwenye vumbi na vilima vya samadi ni watu waliochaguliwa na Mungu.
2 Wanaamini kuwa kama watu wale wangekuwa vyombo vya wokovu Wake Mungu, basi mbingu na ardhi zitageuzwa juu na chini na watu wote watacheka kupindukia. Wanaamini kuwa iwapo Mungu atawachagua watu wasio na sifa yoyote wafanywe viumbe kamili, basi wao walio na sifa watakuwa Mungu Mwenyewe. Maoni yao yamechafuliwa na kutoamini; hakika, mbali na kutoamini, wao ni wanyama wasio na maana. Kwa maana wao wanathamini tu nyadhifa, hadhi kuu na mamlaka; wanachokithamini sana ni makundi makuu na madhehebu makuu. Hawana heshima hata kidogo kwa wale wanaoongozwa na Kristo; wao ni wasaliti tu waliomgeuka Kristo, kuugeuka ukweli na uhai.
3 Ninasema kuwa wote wale wasioenzi ukweli ni wasioamini na waasi wa ukweli. Watu kama hawa hawatawahi kuipokea idhini ya Kristo. Umeweza sasa kutambua kiasi cha kutoamini kilicho ndani yako? Na kiasi gani cha usaliti kwa Kristo? Kwa hivyo Nakuhimiza hivi; Kwa maana umeichagua njia ya ukweli, basi huna budi ila kujitolea na moyo wote; usiwe na kuchanganyikiwa au wa kusitasita. Unafaa kufahamu kuwa Mungu si wa ulimwengu huu au wa mtu yeyote, bali ni wa wale wote wanaoamini katika Mungu kwa kweli, wote wale wanaomwabudu, na wote wale waliojitolea na wanaoamini katika Mungu.
Umetoholewa kutoka katika “Je, Wewe Ni Muumini wa Kweli wa Mungu?” katika Neno Laonekana katika Mwili