925 Mungu Hamruhusu Shetani Kuwadhuru Wale Anaotaka Kuokoa kwa Kupenda

1 Baada ya kuupokea ushuhuda kutoka kwa Ayubu kufuatia mwisho wa majaribio yake, Mungu aliamua kwamba angepata kundi au zaidi ya kundi—la watu kama Ayubu, ilhali aliamua kutowahi tena kumruhusu Shetani kushambulia au kunyanyasa mtu yeyote mwingine kwa kutumia mbinu ambazo kwazo alimjaribu, kumshambulia na kumnyanyasa Ayubu, kwa kufanya mzaha na Mungu; Mungu hakumruhusu Shetani tena kufanya mambo kama hayo kwa binadamu ambaye ni mnyonge, mjinga, na asiyejua—ilikuwa tosha kwamba Shetani alikuwa amemjaribu Ayubu! Kutomruhusu Shetani kuwanyanyasa watu vyovyote anavyotaka ndiyo rehema ya Mungu.

2 Kwani maisha na kila kitu cha watu wanaomfuata Mungu yanatawaliwa na kupangiliwa na Mungu, na Shetani hastahili kutawala waliochaguliwa na Mungu apendavyo—mnafaa kuwa wazi kuhusu hoja hii! Mungu anajali kuhusu unyonge wa binadamu, na kuelewa ujinga na kutojua kwake. Ingawaje, ili binadamu aweze kuokolewa kabisa, lazima Mungu amkabidhi kwa Shetani, Mungu hayuko radhi kumwona tena binadamu akichezewa kama mjinga na kunyanyaswa na Shetani na hataki kumwona binadamu siku zote akiteseka. Binadamu aliumbwa na Mungu, na inaeleweka kikamilifu kwamba Mungu anatawala na anapangilia kila kitu cha binadamu; hili ni jukumu la Mungu na mamlaka ambayo Mungu anatawala mambo yote!

3 Mungu hamruhusu Shetani kunyanyasa na kutumia vibaya binadamu apendavyo, Hamruhusu Shetani kutumia mbinu mbalimbali za kumpotosha binadamu, na vilevile, Hamruhusu Shetani kuingilia kati ukuu wa Mungu kwa binadamu, wala Hamruhusu Shetani kukanyaga na kuangamiza Sheria ambazo Mungu anatawalia mambo yote, kutosema chochote kuhusu kazi kuu ya Mungu ya kusimamia na kuwaokoa wanadamu! Wale ambao Mungu anataka kuokoa na wale ambao wanaweza kuwa na ushuhuda kwa Mungu, ndio msingi na hali halisi ya kazi ya Mungu ya mpango wa usimamizi wa miaka elfu sita, pamoja na bei ya jitihada zake katika kazi yake ya miaka elfu sita. Mungu anawezaje kuwakabidhi watu hawa kwa Shetani hivihivi.

Umetoholewa kutoka katika “Kazi ya Mungu, Tabia ya Mungu, na Mungu Mwenyewe II” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 924 Asili ya Shetani ni Katili na Ovu

Inayofuata: 927 Mamlaka ya Mungu ni Sheria ya Mbingu Ambayo Shetani Hawezi Kuzidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp