366 Wale Wasioweza Kufuata Kazi ya Mungu Wataondolewa

1 Unaviona vitendo hivi vyote vya Mungu sasa, ilhali ungali unapinga na unakuwa mwasi na hutaki kunyenyekea; unayahifadhi mambo mengi ndani yako na unafanya utakacho; unafuata ashiki zako, na kile upendacho—huu ni uasi; huu ni upingaji. Imani katika Mungu ambayo inatekelezwa kwa ajili ya mwili, kwa ajili ya ashiki za mtu, na kwa ajili ya kile anachopenda mtu, kwa ajili ya ulimwengu, na kwa ajili ya Shetani ni chafu; ni upinzani na uasi. Kunazo aina zote tofauti za imani sasa: Baadhi hutafuta hifadhi dhidi ya janga, na wengine hutafuta kupokea baraka, huku baadhi wakitamani kuelewa mafumbo na bado wengine hujaribu kupata pesa. Hiyo yote ni mifumo ya upinzani; hiyo yote ni kukufuru! Kusema kwamba mtu anapinga au anaasi—huku si kwa mujibu wa mambo haya?

2 Watu wengi sasa hivi wanalalamika, wanatamka manung’uniko au kutoa hukumu. Haya yote ni mambo yanayofanywa na waovu; wao ni binadamu wapinzani na waasi. Watu ambao Mungu huwapata ni wale wanaonyenyekea Kwake kabisa, wale waliopotoshwa na Shetani lakini wameokolewa na kushindwa na kazi Yake sasa, wale waliovumilia majaribu na hatimaye wamepokelewa kabisa na Mungu na hawaishi tena katika umiliki wa Shetani na wamevunja minyororo ya udhalimu, walio radhi kuishi kwa kudhihirisha utakatifu—hawa ndio watu watakatifu zaidi; hawa ndio wale watakatifu. Kama matendo yako ya sasa hayalingani na sehemu moja ya mahitaji ya Mungu utaondolewa. Hili halipingiki. Kila kitu kinafanywa kulingana na leo; ingawa Amekuamulia awali na kukuchagua wewe, matendo yako leo bado yataamua matokeo yako. Kama huwezi kuenda sambamba sasa, utaondolewa.

Umetoholewa kutoka katika “Unapaswa Kujua Namna Ambavyo Binadamu Wote Wameendelea Hadi Siku ya Leo” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 365 Asili Yako ni Potovu Sana

Inayofuata: 367 Mungu Huwaokoa Watu Kutoka katika Maisha ya Mateso Duniani

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp