683 Mtu Hawezi Kuja Kumjua Mungu kwa Kufurahia Neema Yake

1 Kwamba mwanadamu anaweza kuteseka kwa ajili ya Mungu na ameweza kufikia umbali huu ni, kuhusiana na jambo moja, kwa sababu ya upendo wa Mungu, na kuhusiana na jambo lingine, ni kwa sababu ya wokovu wa Mungu; zaidi ya hayo, ni kwa sababu ya kazi ya hukumu na kuadibu ambayo Mungu ametekeleza ndani ya mwanadamu. Kama hamna hukumu, kuadibu, na majaribio ya Mungu, na kama Mungu hajawafanya mteseke, basi, kusema ukweli, ninyi hammpendi Mungu kweli. Kadri kazi ya Mungu ilivyo kuu zaidi ndani ya mwanadamu, na kadri mateso ya mwanadamu yalivyo makuu zaidi, ndivyo inavyoweza kuonyesha zaidi hasa vile kazi ya Mungu ilivyo ya maana, na ndivyo moyo wa mwanadamu unavyoweza kumpenda Mungu kweli zaidi.

2 Leo mwanadamu huona kwamba na neema, upendo na rehema ya Mungu pekee, hana uwezo wa kujijua mwenyewe kweli, sembuse kuweza kujua kiini cha mwanadamu. Ni kupitia tu usafishaji na hukumu ya Mungu, ni wakati tu wa usafishaji kama huo ndiyo mwanadamu anaweza kujua kasoro zake, na kujua kwamba hana chochote. Hivyo, upendo wa mwanadamu kwa Mungu umejengwa juu ya msingi wa usafishaji na hukumu ya Mungu. Kama wewe hufurahia tu neema ya Mungu, na maisha ya familia yenye amani au baraka yakinifu, basi hujampata Mungu, na imani yako kwa Mungu haiwezi kuchukuliwa kama iliyofaulu.

3 Mungu tayari ametekeleza hatua moja ya kazi ya neema katika mwili, na tayari amempa mwanadamu baraka yakinifu—lakini mwanadamu hawezi kufanywa mkamilifu na neema, upendo, na rehema pekee. Katika uzoefu wa mwanadamu yeye hukabiliwa na baadhi ya upendo wa Mungu, na huuona upendo na rehema ya Mungu, lakini baada ya kupitia kwa kipindi fulani cha wakati, yeye huona kwamba neema ya Mungu na upendo na rehema Yake hayawezi kumfanya mwanadamu awe mkamilifu, na hayana uwezo wa kufichua kile ambacho ni potovu ndani ya mwanadamu, wala hayawezi kumwondolea mwanadamu tabia yake potovu, au kufanya kuwa kamilifu upendo na imani yake. Kazi ya Mungu ya neema ilikuwa kazi ya kipindi kimoja, na mwanadamu hawezi kutegemea kufurahia neema ya Mungu ili kumjua Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Ni kwa Kupitia tu Majaribio ya Kuumiza Ndiyo Mnaweza Kujua Kupendeza kwa Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 682 Mungu Amkamilisha Mwanadamu kwa Njia Nyingi

Inayofuata: 684 Wote Wamtafutao Mungu kwa Kweli Wanaweza Kupata Baraka Zake

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp