363 Watu Hawajui Jinsi Walivyo Duni

1 Katika akili za wanadamu, Mungu si mwandani kwao, lakini Yule ambaye daima huwalaani; kwa hivyo, wanadamu hawamtilii maanani, hawamkaribishi, kila mara wao huwa hasimu Kwake, na hili halijawahi kubadilika kamwe. Kwa sababu wanadamu wana mambo haya katika mioyo yao, Mungu asema wanadamu hawana akili na ni waovu, na kwamba hata hisia ambazo wanadamu kwa kuwazia wamejizatiti nazo haziwezi kuonekana ndani yao. Wanadamu hawadhihirishi fikira yoyote kwa hisia za Mungu, lakini hutumia kinachoitwa “haki” kumshughulikia Mungu.

2 Wanadamu wamekuwa hivi kwa miaka mingi na kwa sababu hii Mungu amesema tabia yao haijabadilika. Inaweza kusemwa kwamba wanadamu ni wanyonge wasio na thamani kwa sababu hawajithamini. Kama hata hawajipendi, bali hujikandamiza, hili halionyeshi kwamba hawana thamani? Wanadamu ni kama mwanamke mwovu ambaye hujihadaa na ambaye hujitoa kwa wengine kwa hiari kuingiliwa bila heshima. Lakini hata hivyo, bado hawajui vile walivyo duni. Wao hufurahia kuwatumikia wengine, au kuzungumza na wengine, kujiweka chini ya utawala wa wengine; huu kweli si uchafu wa wanadamu?

3 Kwa sababu wanadamu hawajijui, dosari yao kubwa sana ni kuonyesha kwa hiari haiba yao mbele ya wengine, wakionyesha sura yao mbaya; Hiki ni kitu ambacho Mungu hukichukia zaidi. Kwa sababu mahusiano kati ya watu si ya kawaida, na hakuna mahusiano ya kawaida ya mtu mmoja na mwingine kati ya watu, sembuse uhusiano wa kawaida kati yao na Mungu. Mungu amesema mengi sana, na kwa kufanya hivyo lengo Lake kuu ni kumiliki nafasi ndani ya mioyo ya wanadamu, kuwafanya watu waondoe sanamu zote ndani ya mioyo yao, ili Mungu aweze kuwatawala wanadamu wote na Atimize lengo Lake la kuwa duniani.

Umetoholewa kutoka katika “Sura ya 14” ya Ufafanuzi wa Mafumbo ya Maneno ya Mungu kwa Ulimwengu Mzima katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 362 Mungu Hamruhusu Kiumbe Yeyote Kumdanganya

Inayofuata: 364 Wewe ni Mwasi Sana

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp