767 Kumwamini Mungu Lakini Kutompenda ni Maisha Matupu

1 Hakuna funzo lililo kubwa kuliko lile la kumpenda Mungu, na inaweza kusemwa kuwa funzo ambalo watu hujifunza katika maisha yao yote ya imani ni jinsi ya kumpenda Mungu. Hii ni kusema, kama unamwamini Mungu ni lazima umpende Mungu. Ikiwa unamwamini tu Mungu lakini humpendi, hujapata ufahamu wa Mungu, na hujawahi kumpenda Mungu kwa upendo wa kweli utokao moyoni mwako, basi imani yako kwa Mungu ni bure; kama katika imani yako kwa Mungu humpendi Mungu, basi unaishi bure, na maisha yako yote ndiyo ya duni zaidi kwa maisha yote. Ikiwa katika maisha yako yote hujawahi kumpenda au kumtosheleza Mungu, basi kuna haja gani ya kuishi? Kuna haja gani ya imani yako kwa Mungu? Huku si kuharibu nguvu?

2 Kama watu wanataka kuamini na kumpenda Mungu, ni sharti wagharamike. Badala ya kujaribu kuenenda kwa namna fulani kwa nje tu, wanapaswa watafute utambuzi wa kweli kutoka ndani ya mioyo yao. Ikiwa unapenda sana kuimba na kucheza lakini huwezi kuonyesha ukweli katika vitendo, unaweza kusemekana kwamba unampenda Mungu? Kumpenda Mungu kunahitaji utafutaji wa mapenzi ya Mungu katika mambo yote, na kwamba ujisaili wewe mwenyewe kwa kina jambo lolote likikutokea, kujaribu kujua mapenzi ya Mungu na kujaribu kuona mapenzi ya Mungu ni yapi katika suala hili, Anataka ufanikishe nini, na ni jinsi gani utayajali mapenzi Yake?

Umetoholewa kutoka katika “Kumpenda Mungu tu Ndiko Kumwamini Mungu Kweli” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 766 Wito wa Wale Wampendao Mungu

Inayofuata: 768 Kuishi Kutekeleza Mapenzi ya Mungu ni Jambo la Maana Zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp