624 Mungu Hawasifu Wale Wanaohudumu Kama Paulo

Kama wale wanaomhudumia Mungu watafuata hulka yao na kutenda kulingana na mapenzi yao binafsi, basi wamo katika hatari ya kutupwa nje wakati wowote. Wale wanaotumia miaka yao mingi ya uzoefu kwa kumhudumia Mungu ili kutega mioyo ya watu, kuwasomea na kuwadhibiti, kujiinua wao wenyewe—na wale katu hawatubu, katu hawakiri dhambi zao, katu hawakatai manufaa ya cheo—watu hawa wataanguka mbele ya Mungu. Hawa ni watu walio kama Paulo, waliojaa majivuno ya vyeo vyao na wanaoonyesha ukubwa wao. Mungu hatawakamilisha watu kama hawa. Aina hii ya huduma huzuia kazi ya Mungu. Watu wanapenda kushikilia vitu vya kale. Wanashikilia fikira za kale, wanashikilia vitu vya kale. Hiki ni kizuizi kikuu katika huduma yao. Kama huwezi kuvitupa vitu hivi, vitu hivyo vitayakaba maisha yako yote. Mungu hatakupongeza, hata kidogo, hata kama utaivunja miguu yako au mgongo wako ukitia bidii, au hata ukifa katika “huduma” ya Mungu. Kinyume cha mambo ni kwamba: Atasema kwamba wewe ni mtenda maovu.

Umetoholewa kutoka katika “Njia ya Huduma ya Kidini lazima Ipigwe Marufuku” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 623 Tabia ya Aina Hii Inaweza Kufaa kwa Huduma ya Mungu?

Inayofuata: 625 Bila Kumjua Mungu, Utamkosea Mungu kwa Urahisi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp