534 Kutofuatilia Ukweli Huishia Katika Kulia na Kusaga Meno Daima

1 Kuna watu wengi wasiofuatilia uzima; hata kama kuna wengine, idadi hiyo inaweza kuhesabiwa kwa vidole vya mtu. Watu wanahangaishwa sana kuhusu siku zao za baadaye na hawatilii maanani uzima kwa vyovyote vile. Watu wengine huasi dhidi ya Mungu na kumpinga, humhukumu bila Yeye kufahamu na hawatendi ukweli. Siwajali watu hawa kwa sasa, na Najizuia kushughulikia tabaka hili la wana wa uasi kwa sasa. Katika siku za usoni utaishi gizani, ukilia na kusaga meno yako. Wewe huhisi thamani ya nuru unapoishi ndani yake, lakini utatambua thamani yake mara tu unapoishi katika usiku wa giza. Utasikitika wakati huo. Ni kwa sababu bado huelewi kazi ya sasa ndio unakosa kutunza wakati wako sasa. Mara tu kazi ya ulimwengu mzima ianzapo, kumaanisha wakati ambapo kila kitu Nisemacho leo kimetimia, watu wengi watakuwa wakishikilia vichwa vyao kwa kilio cha uchungu. Je, huko sio kuingia katika giza na kulia na kusaga meno?

2 Watu wote ambao hufuatilia uzima kweli na wamefanywa kuwa kamili watatumiwa, huku wana wote wa uasi ambao hawafai kutumiwa wataingia gizani, bila kupokea kazi yoyote ya Roho Mtakatifu kwa vyovyote vile na kubaki wasioweza kufahamu chochote. Hivyo wataingia katika adhabu kuomboleza na kutokwa na machozi. Kama umejiandaa vyema katika awamu hii ya kazi na maisha yako yamekomaa, basi wewe ni mtu unayefaa kutumiwa. Kama umejiandaa vibaya, basi hata kama umejitayarisha kwa awamu inayofuata ya kazi utakuwa hufai. Wakati huo, hata kama utataka kujiandaa mwenyewe, nafasi itakuwa imepita. Mungu atakuwa ameondoka; utaenda wapi basi kutafuta aina ya nafasi iliyo mbele yako sasa, na utaenda wapi basi kupokea zoezi linalotolewa na Mungu binafsi? Wakati huo, haitakuwa Mungu akinena binafsi au akitoa sauti Yake. Utaweza tu kusoma kinachosemwa leo; utawezaje kuelewa kwa urahisi? Ni vipi ambavyo maisha ya baadaye yataweza kulingana na ya leo? Wakati huo, kulia na kusaga meno kwako hakutakuwa kupitia kifo kilicho hai?

Umetoholewa kutoka katika “Ukweli wa Ndani wa Kazi ya Ushindi (1)” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 533 Yeyote Asiyetenda Ukweli Ataondolewa

Inayofuata: 535 Wale Wasiofuatilia Ukweli Watajuta

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp