719 Wale Wanaotii Kazi ya Mungu kwa Kweli Wanaweza Kupatwa na Yeye

1 Kuwa na ushahidi mkuu kwa Mungu hasa kunahusiana na ikiwa una ufahamu wa Mungu wa vitendo au la, na ikiwa unaweza au huwezi kutii mbele ya mtu huyu ambaye ni wa kawaida na kutii mpaka hata kifo. Ikiwa unamshuhudia Mungu kwa kweli kupitia utii huu, hiyo inamaanisha kuwa umepatwa na Mungu. Kuwa na uwezo wa kutii mpaka kifo, na kuwa bila malalamiko mbele Yake, kutohukumu, kutokashifu, kutokuwa na mawazo, na kutokuwa na makusudi mengine—kwa njia hii Mungu atapata utukufu. Utiifu mbele ya mtu wa kawaida ambaye anadharauliwa na mwanadamu na kuwa na uwezo wa kutii mpaka kifo bila mawazo yoyote—huu ni ushuhuda wa kweli.

2 Uhakika ambao Mungu anataka watu waingie ndani ni kwamba unaweza kutii maneno Yake, unaweza kuweka maneno Yake katika matendo, kuweza kuinama mbele ya Mungu wa vitendo na kujua upotovu wako mwenyewe, kuweza kufungua moyo wako mbele Yake, na mwishowe kupatwa na Yeye kupitia maneno haya Yake. Mungu hupata utukufu wakati maneno haya yanakushinda na kukufanya uwe mtiifu kikamilifu Kwake; kwa njia hii Anamwaibisha Shetani na kukamilisha kazi Yake. Wakati huna mawazo yoyote ya utendaji wa Mungu mwenye mwili, yaani, unaposimama imara katika jaribio hili, basi wewe huwa na ushuhuda mzuri.

3 Ikiwa kuna siku ambayo uko na uelewa mkamilifu juu ya Mungu wa matendo na unaweza kutii mpaka kifo kama Petro, utapatwa na Mungu, na kukamilishwa na Yeye. Ni kwa sababu ya utendaji wa Mungu ndiyo maana watu wote wako katikati ya majaribio; kazi Yake ni ya vitendo, siyo ya kawaida. Kwa kuelewa kikamilifu maneno Yake ya vitendo, matamshi Yake ya vitendo bila mawazo yoyote, na kuwa na uwezo wa kumpenda kwa kweli zaidi ndivyo kazi Yake ilivyo ya vitendo zaidi, utapatwa na Yeye. Kundi la watu ambao Mungu atapata ni wale wanaomjua Mungu, yaani, ambao wanajua utendaji Wake, na hata zaidi ni wale wanaoweza kutii kazi ya vitendo ya Mungu.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Wanaompenda Mungu Kwa Kweli Ni Wale Wanaoweza Kutii Utendaji Wake Kabisa” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 718 Kuwa na Imani Katika Mabadiliko ya Tabia

Inayofuata: 720 Mungu Ataka Utiifu wa Kweli wa Mwanadamu

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

418 Umuhumi wa Maombi

Sala ni mojawapo ya njia ambazo mwanadamu hutumia kushirikiana na Mungu, ni njia ambayo mwanadamu hutumia kumwita Mungu, na ni mchakato...

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp