Sura ya 106

Wale wasioyajua maneno Yangu, wale wasioujua ubinadamu Wangu wa kawaida, na wale wanaokataa uungu Wangu wote wataangamizwa hadi wasikuwepo. Hakuna atakayeachiliwa kutokana na hili, na wote lazima wafikie kipengele hiki kwa njia ya kuridhisha, kwa sababu ni amri Yangu ya utawala, na hiki ndicho kifungu cha uzito zaidi cha kuweka fanya kwa matendo. Wale wasioyajua maneno Yangu ni wale ambao wamesikiliza yale ambayo Nimesema wazi, ilhali bado hawayajui, kwa maneno mengine wale ambao hawaelewi masuala ya kiroho (kwa kuwa Sijaumba sehemu hii ya mwili kwa ajili ya wanadamu, Sihitaji mengi kutoka kwao; Nahitaji tu kwamba wasikilize maneno Yangu na kisha wayaweke katika matendo). Wao sio watu wa nyumba Yangu, sio wa aina moja na Mimi; ni wa ufalme wa Shetani. Kwa hivyo simtaki hata mmoja wa hao watu wasioelewa masuala ya kiroho. Hapo awali, mlifikiria Nilikuwa nimezidi; leo mtaelewa. Wanyama watawezaje kuzungumza na Mungu? Huo si upuuzi? Wale wasiojua ubinadamu Wangu wa kawaida ni wale ambao wanatumia fikira zao wenyewe kupima Nifanyacho katika ubinadamu Wangu. Badala ya utiifu, wao, kwa macho yao ya kimwili, wanajaribu kunikosoa Mimi mambo madogo madogo. Pengine Nimenena bure? Nilisema ubinadamu Wangu wa kawaida ni sehemu Yangu ya lazima, Mungu mkamilifu Mwenyewe, na hii ni njia halisi ambayo ubinadamu Wangu wa kawaida na uungu kamili unafanya kazi kwa pamoja: Wakati ambapo vitu Nifanyavyo kupitia kwa ubinadamu Wangu wa kawaida havipatani na dhana za mwanadamu, wale wanaonikataa na wale wasiolingana na Mimi wanafichuliwa. Baada ya haya, uungu Wangu kamili unanena kupitia katika ubinadamu, na kwa njia hii, Nimewashughulikia watu wengine kwa namna hii. Kama huelewi Ninachofanya lakini hata hivyo unatii, mtu wa aina hii Simshutumu, ila Nampa nuru. Huyu ni aina ya mtu Ninayempenda, na kwa sababu ya utiifu wako Nakupa nuru. Wale wanaokataa uungu Wangu ni pamoja na wale ambao hawajui maneno Yangu, wale ambao hawalingani na ubinadamu Wangu wa kawaida, na wale ambao hawapendi Ninachofanya katika uungu (kwa mfano, kukasirika Kwangu au ujenzi wa kanisa na kadhalika). Hayo yote ni maonyesho ya kukataa uungu Wangu. Lakini kuna kitu kimoja Ninachosisitiza na kila mmoja wenu lazima awe makini: Watu ambao hawalingani na mtu ambaye Niliye leo wanapinga uungu Wangu. Mbona Naendelea kusema kuwa mtu amabye Niliye ni Mungu Mwenyewe mkamilifu? Tabia ya mtu amabaye Niliye ni inajumuisha ujumla wa tabia takatifu; usitumie fikra za wanadamu kunipima Mimi. Hata sasa, watu wengi bado wanasema kuwa Nina ubinadamu wa kawaida na hivyo vitu Nifanyavyo sivyo sahihi vyote. Watu hawa—je, hamjitafutii kufa? Hawajui neno hata moja ya yale Ninayosema, na ni ukoo wa vipofu kabisa, wazawa wa joka kuu jekundu. Nitawaambia kila mmoja mara nyingine (na Sitasema tena baada ya hapo, yeyote akikiuka hili tena, kwa hakika atalaaniwa): Maneno Yangu, kicheko Changu, kula Kwangu, kuishi Kwangu, usemi Wangu na tabia yote yanafanywa na Mimi—Mungu Mwenyewe, na hakuna dalili hata kidogo ya mwanadamu iliyochanganyika ndani, hakuna! Hakuna kabisa! Kila mtu anapaswa kukoma kucheza michezo yake ya akili, koma na hesabu zako ndogo ndogo. Kadiri unavyoendelea na hili zaidi ndivyo utakavyoangamia zaidi. Sikia ushauri Wangu!

Kila mara Naangalia ndani zaidi ya moyo wa kila mmoja, Naangalia kila moja ya neno na tendo lake, na naona kwa wazi, mmoja baada ya mwingine, wale Ninaowapenda na wale Nisiowapenda. Hili ni jambo ambalo watu hawawezi kufikiria, na hata zaidi, jambo ambalo watu hawawezi kutimiza. Nimesema mengi sana na Nimefanya vitu vingi sana; ni nani angeweza kunena wazi juu ya ni nini malengo Yangu kwa matamshi Yangu, na kwa kazi Yangu? Hakuna anayeweza kunena kuyahusu kwa wazi. Baada ya hii, Sitanena zaidi; kwa upande moja hii itawaangamiza watu wote ambao Siwapendi, na kwa upande mwingine, itawafanya mteseke zaidi kidogo kuhusu hii, ili kwa mara nyingine mpate kupitia ufufuo kutoka kwa wafu lakini na ukali zaidi. Hili haliwezi kuamuliwa na watu, na hakuna anayeweza kuliepa. Hata kama unajua kuhusu haya sasa, wakati utakapofika bado hutaweza kuepuka mateso haya, kwa sababu hivi ndivyo Nafanya kazi. Lazima Nifanye kazi hivi ili Nifikie malengo Yangu, na ili Niache mapenzi Yangu yatimike kwenu. Hii ndiyo sababu yanaitwa “mateso ya mwisho ambayo lazima upitie.” Mwili wenu hautateseka tena baadaye, kwa sababu joka kuu jekundu litakuwa limeangamizwa na Mimi, na halitathubutu kuleta ghasia tena. Hii ndiyo hatua ya mwisho kabla ya kuingia katika mwili; ni hatua ya mpito. Lakini msiogope, bila shaka Nitawaongoza kwa mgogoro baada ya mgogoro. Amini kuwa Mimi ni Mungu mwenye haki Mwenyewe. Kile ambacho Nimesema kitatimizwa kwa hakika. Mimi ni Mungu mwaminifu Mwenyewe. Mataifa yote, nchi zote, na madhehebu yote yanarejea Kwangu na kukusanyika kwa kiti Changu cha enzi. Hii ni nguvu Yangu kubwa, na Nitamhukumu kila mwana muasi, Nikiwatupa katika ziwa la moto na kiberiti, bila ubaguzi wowote, wote lazima wajiondoe. Hii ndiyo hatua ya mwisho ya mpango Wangu wa usimamizi, na wakati ambapo hii itakamilika, Nitaingia katika mapumziko, kwa sababu kila kitu kitakuwa kimefanyika, na mpango Wangu wa usimamizi utakuwa umefika mwisho.

Kwa sababu kasi ya kazi Yangu imeongezeka (ingawa moyo Wangu hauna wasiwasi), Nafichua maneno Yangu kwenu kila siku, Nafunua mafumbo Niliyo nayo kwenu kila siku, ili mfuate kwa karibu nyayo Zangu. (Hii ni busara Yangu, kutumia maneno Yangu kuwakamilisha watu, lakini pia kuwaangamiza watu. Wote wanasoma maneno Yangu, na wanaweza kutenda kulingana na mapenzi Yangu katika maneno Yangu. Wale walio hasi watakuwa hasi, wale ambao wanafaa kufichuliwa wataonyesha tabia zao za kweli, wanaokataa watakataa, na wale wanaonipenda kwa uaminifu watakuwa waaminifu hata zaidi. Kwa hivyo, wote wanaweza kufuata nyayo Zangu. Hali kadhaa Nilizoeleza zote ni mbinu za jinsi Ninavyofanya kazi na ni malengo Ninayotaka kufikia). Hapo awali Nimesema: Haijalishi Ninavyowaongoza, mnafaa kufuata kwa njia iyo hiyo; chochote Ninachowaambia, mnafaa kusikia. Nilimaanisha nini Nikisema hili? Je mnajua? Lengo na umuhimu wa neno Langu ni nini? Je mnaelewa? Ni watu wangapi wanaweza kueleza hili kwa ufasaha kikamilifu? Ninaposema “Haijalishi Ninavyowaongoza, mnafaa kutafutata kwa njia iyo hiyo,” Simaanishi tu uongozi Wangu Ninaowapa kama mtu Niliye; aidha Ninaashiria maneno Ninenayo na njia Ninayopitia. Leo, neno hili limekamilika kweli. Baada tu ya kunena maneno Yangu, aina yote ya nyuso za kipepo inawekwa wazi mbele ya mwanga wa uwepo Wangu, ili muweze kuiona yote kwa wazi. Neno hili Langu silo tu tangazo kwa Shetani, ila ni kuaminiwa kwa ninyi wote. Wengi wenu mnapuuza neno hili, mkiliamini kuwa ni kuaminiwa kwa ninyi, lakini hamgundui kuwa hili ni neno la hukumu, neno ambalo linabeba mamlaka. Lengo la maneno Yangu ni kumwamuru Shetani kunifanyia Mimi huduma vizuri na kunitii kabisa. Katika mafumbo Niliyofichua hapo zamani, bado kuna mengi ambayo hamwelewi bado, kwa hivyo baadaye Nitawafichulia mengi zaidi, ili muweze kuwa na uelewa wazi na mkamilifu kabisa.

Majanga yanapokuja, kila mtu anahofu. Watu wote hulia kwa huzuni na kuhisi chuki ya mambo maovu waliyotenda zamani, lakini kufikia wakati huo watakuwa wamechelewa sana, kwani hii ni enzi ya ghadhabu. Sio wakati wa kuokoa watu na kutoa neema, ila ni wakati wa kuwaondoa watendaji huduma wote na kuwacha wana Wangu kutawala kwa niaba Yangu. Kwa kweli hii ni tofauti na zamani, na haijawahi kutokea kutoka uumbaji wa dunia. Kwa sababu Nimeumba dunia mara moja, Nitaangamiza dunia mara moja, na yale ambayo Nimeamua kabla hayawezi kubadilishwa na yeyote. Maneno haya mawili “ushirika wa wanadamu Wakristo” na “ushirika wa wanadamu wote wapya” yalitajwa mara nyingi awali. Yanafaa kuelezwa vipi? Je, ushirika wa wanadamu Wakristo unaashiria wazaliwa wa kwanza? Je, ushirika wa wanadamu wote wapya unaashiria pia wazaliwa wa kwanza? Hapana, watu hawajaitafsiri barabara. Kwa sababu dhana za binadamu zinaweza tu kuelewa vitu kwa kiwango hiki, Nitaweka hili wazi hapa na sasa kwenu. Ushirika wa wanadamu Wakristo na ushirika wa wanadamu wote wapya sio sawa; maana yao ni tofauti. Ingawa kwa maneno haya mawili hayana tofauti sana, na yanaweza kuonekana kuwa kitu kimoja, hali ya kweli ni kinyume kabisa. Ushirika wa wanadamu Wakristo unaashiria akina nani hasa? Ama wao wanaashiria nini? Tukiongelea wanadamu Wakristo, kila mmoja atanifikiria Mimi. Wote hawajakosea kabisa kufanya hivi. Zaidi, katika dhana za wanadamu, neno “wanadamu” bila shaka linaashiria wanadamu, na hakuna mtu hata mmoja anayeweza kulishirikisha na kitu kingine. Tunapoongelea “ushirika,” watu wanaweza kufikiria huu ni mkusanyiko wa watu wengi na karibu ni kitengo kimoja, kwa hivyo unaitwa ushirika. Hapa inaweza kuonekana kuwa akili za mwanadamu ni sahili sana, na haziwezi kuelewa kusudi Langu kabisa. Sasa, Nitaanza rasmi kushiriki kuhusu ushirika wa wanadamu Wakristo ni akina nani (lakini kila mmoja lazima aweke kando dhana zake, la sivyo hakuna atakayeweza kuelewa, na hata kama Ningeeleza neno hilo, watu hawangeliamini, wala kulielewa): Baada tu ya maneno Yangu kunenwa, wazaliwa Wangu wa kwanza wote wataweza kutenda kulingana na mapenzi Yangu, na kuonyesha mapenzi Yangu, ili kwamba wawe ni wa moyo mmoja na wa kunena jambo moja. Wanapohukumu mataifa yote na watu wote, wataweza kutekeleza haki Yangu, na kutekeleza amri Zangu za utawala; wao ni maonyesho Yangu, na ni udhihirisho Wangu. Hivyo, inaweza kusemekana kuwa ushirika wa wanadamu Wakristo ni tendo la hakika la wana wazaliwa wa kwanza kutekeleza amri Zangu za utawala, wao ni mamlaka katika mikono ya wazaliwa wa kwanza; na hili lote linahusiana na Kristo, ndio sababu ya neno wanadamu Wakristo. Zaidi, wazaliwa wa kwaza wote wanaweza kutenda kulingana na mapenzi Yangu, kwa hivyo Ninatumia neno ushirika. Ushirika wa wanadamu wote wapya unamaanisha watu wote walio katika jina Langu, kwa maneno mengine, wazaliwa Wangu wa kwanza, wana Wangu, na watu Wangu. “Wapya” linaashiria jina Langu. Kwa sababu wako katika jina Langu (Jina Langu linabeba kila kitu, na ni jipya milele na halizeeki kamwe, halibadilishwi na mwanadamu), na wao watabaki hai milele baadaye, wao ni watu wapya wa ulimwengu. “Ushirika” hapa linahusu idadi ya watu, na sio sawa na hali ya awali. Wakati neno Langu linanenwa, wote lazima waliamini. Usiwe na shaka. Ondoa dhana zako za kibinadamu na fikira za kibinadamu. Mchakato Wangu wa sasa wa kufichua mafumbo ni hasa mchakato wa kutoa dhana za kibinadamu na fikira (kwa sababu watu hutumia dhana zao kunipima Mimi na kupima Ninachosema, Ninatumia mafumbo Yangu Mwenyewe yaliyofichuliwa kutoa dhana za kibinadamu na kutoa fikira za kibinadamu). Kazi hii itakamilika hivi karibuni. Mafumbo Yangu yanapofichuliwa kwa hatua fulani, watu hawatakuwa na michakato ya mawazo kuhusu maneno Yangu na watakoma kutumia dhana zao za kibinadamu kunipima Mimi. Kile wanachofikiria kila siku, Nitafichua, na Nitalipiza kisasi. Katika hatua fulani, watu hawatafikiria tena, vichwa vyao vitakuwa tupu bila mawazo yoyote, na watatii maneno Yangu kabisa, na hapo ndipo utaingia katika ulimwengu wa kiroho. Hii ni hatua katika kazi Yangu kabla ya kuwaruhusu mwingie katika ulimwengu wa kiroho. Lazima mwondoe dhana za kibinadamu kabla ya kuweza kuwa mtakatifu na bila dosari na kuingia katika ulimwengu wa kiroho, na hii ndiyo maana asili ya “Mimi ni mwili mtakatifu wa kiroho.” Lakini lazima mtende kulingana na hatua Zangu, na kabla ya ninyi kutambua, wakati Wangu utakuja.

Iliyotangulia: Sura ya 105

Inayofuata: Sura ya 107

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp