710 Tabia Yako Inaweza Kubadilika Tu kwa Kutii Kazi ya Mungu

1 Ikiwa unaweza kufuata maneno halisi ya Roho Mtakatifu katika uzoefu wako wa utendaji, utaweza kutimiza mabadiliko katika tabia yako. Ikiwa utafuata na kutafuta chochote ambacho Roho Mtakatifu husema, wewe ni mtu anayemtii Yeye, na kwa njia hii utaweza kuwa na mabadiliko katika tabia. Tabia ya mwanadamu hubadilika na maneno halisi ya Roho Mtakatifu; ikiwa kila mara wewe hutetea uzoefu wako wa zamani na sheria, tabia yako haitabadilika. Na hivi sasa suala muhimu zaidi ni kufuata uongozi wa Roho Mtakatifu. Unafuata chochote asemacho Mungu; unatii chochote asemacho Yeye. Watu hawawezi kubadilisha tabia yao wenyewe; lazima wapitie hukumu na kuadibu, mateso na usafishaji wa maneno ya Mungu, au kushughulikiwa, kufunzwa nidhamu, na kupogolewa na maneno Yake. Ni baada ya hapo tu ndipo wanaweza kutimiza utiifu na ibada kwa Mungu, na wasijaribu tena kumdanganya Yeye na kumshughulikia kwa uzembe.

2 Ni kupitia kwa usafishaji wa maneno ya Mungu ndio watu hupata mabadiliko katika tabia. Ni wale tu wanaopitia mfichuo, hukumu, kufundishwa nidhamu, na kushughulikiwa kwa maneno Yake ambao hawatathubutu tena kufanya mambo kwa kutojali, na watakuwa watulivu na makini. Jambo muhimu sana ni kwamba wanaweza kutii neno la sasa la Mungu na kutii kazi ya Mungu, na hata kama hayalingani na fikira za binadamu, wanaweza kuweka kando fikira hizi na kutii kwa hiari. Mabadiliko katika tabia yalipozungumziwa hapo awali, imekuwa hasa kuhusu kujinyima mwenyewe, kuruhusu mwili kuteseka, kufunza nidhamu mwili wa mtu, na kujiondolea mapendeleo ya mwili—hii ni aina moja ya mabadiliko katika tabia. Watu sasa wanajua kwamba maonyesho halisi ya mabadiliko katika tabia ni kutii maneno halisi ya Mungu na vilevile kuweza kuwa na ufahamu halisi wa kazi Yake mpya. Kwa njia hii, ufahamu wa awali wa watu kumhusu Mungu, ambao ulipotoshwa na fikira zao wenyewe, na kutimiza ufahamu wa kweli wa na utiifu Kwake. Hii tu ndio maonyesho halisi ya mabadiliko katika tabia.

Umetoholewa kutoka katika “Wale Ambao Tabia Zao Imebadilika ni Wale Ambao Wameingia Katika Uhalisi wa Neno la Mungu” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 709 Tafuta Ukweli ili Upate Mabadiliko Katika Tabia

Inayofuata: 711 Matendo Mazuri si Sawa na Badiliko Katika Tabia

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp