883 Ni Wakati Tu Ambapo Mungu Alipata Mwili Ndipo Mwanadamu Akawa na Nafasi ya Wokovu

1 Siku moja, uzoefu wenu utakuwa kana kwamba mtaelewa kuwa kupata mwili kwa Mungu—mwili wa binadamu wa kawaida—ndiko kunakohitajiwa na wanadamu wote. Kadiri kupata mwili kwa Mungu, ubinadamu, na chote Anachofichua kinavyozidi kuwa cha kawaida, ndivyo wokovu wetu unavyozidi kuwa mkubwa, na kadiri vitu hivyo vinavyozidi kuwa vya kawaida, ndivyo vinavyozidi kuwa vile tunavyohitaji; kama kupata mwili kwa Mungu kungekuwa kusiko kwa kawaida, basi hakuna hata mmoja wetu—hata ingawa tulichaguliwa na Mungu—ambaye angeweza kuokolewa. Ni hasa kwa sababu ya unyenyekevu na kujificha kwa Mungu, kwa sababu ya hali ya kawaida na ya vitendo ya Mungu huyu anayeonekana asiye wa ajabu, ndiyo watu wanayo nafasi ya wokovu. Ndani ya watu kuna uasi, na kiini cha tabia potovu ya kishetani, na kwa sababu ya hili, kila aina ya dhana, suitafahamu, na uhasama kwa Mungu husababishwa; hata ni kweli kwamba, kwa sababu ya dhana hizi, watu humkana Kristo huyu mara kwa mara, na hukana ubinadamu Wake wa kawaida—ambalo ni kosa kubwa.

2 Ikiwa unatamani kupokea wokovu wa Mungu, na hukumu na kuadibu kwa Mungu, lazima kwanza usahau dhana zako mbalimbali na ufafanuzi wako usio sahihi kumhusu Kristo, lazima usahau utambuzi na maoni yako mbalimbali juu ya Kristo, na lazima ukubali yote yatokayo Kwake. Wakati huo tu ndipo maneno Azungumzayo na ukweli Aonyeshao hutapata uingiaji kiasi katika moyo wako na kuwa maisha yako. Ikiwa unataka kumfuata Kristo, unapaswa kukubali yote yanayohusiana na Yeye; hupaswi kusimama dhidi Yake, hupaswi kushikilia dhana zako mwenyewe na kumwelewa visiyo na kumshuku siku zote, au hata kumpinga na kumkataa. Ukiwa na mtazamo kama huo, unaweza tu kujiumiza; hauna faida hata kidogo kwako.

Umetoholewa kutoka katika “Ni Wakati tu Unapotatua Dhana Zako Ndipo Unaweza Kuingia Kwenye Njia Sahihi ya Imani Katika Mungu I” katika Kumbukumbu za Hotuba za Kristo

Iliyotangulia: 882 Mungu ametoa upendo Wake wote kwa watu

Inayofuata: 884 Upendo wa Mungu Ni wa Kweli Zaidi

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp