295 Binadamu wa Asili Walikuwa Viumbe Wanaoishi Walio na Roho

1 Hapo mwanzo, Nilimuumba mwanadamu, yaani, Nilimuumba babu wa binadamu, Adamu. Alijaliwa na umbo na sura, mwenye kujawa na uhai, kujawa na nguvu ya maisha, na isitoshe, pamoja na utukufu Wangu. Hiyo ilikuwa ni siku tukufu Nilipomuumba mwanadamu. Baada ya hapo, Hawa alitengenezwa kutoka katika mwili wa Adamu, naye alikuwa pia babu wa binadamu, na hivyo watu niliowaumba walikuwa wamejazwa na pumzi Yangu na kujazwa na utukufu Wangu.

2 Adamu kiasili aliumbwa kutoka kwa mkono Wangu na alikuwa akiwasilisha mfano Wangu. Hivyo maana ya asili ya “Adamu” ilikuwa kiumbe kilichoumbwa na Mimi, kilichojawa na nishati Yangu ya uhai, kilichojawa utukufu Wangu, kinacho sura na umbo, kinacho roho na pumzi. Alikuwa kiumbe wa pekee, aliyemilikiwa na roho, ambaye aliweza kuniwakilisha Mimi, kuwa na picha Yangu, na kupokea pumzi Yangu.

3 Hapo mwanzo Hawa alikuwa mtu wa pili kujazwa na pumzi ambaye uumbaji wake nilikuwa nimeamuru, hivyo maana asili ya “Hawa” ilikuwa kiumbe ambaye angeendeleza utukufu Wangu, aliyejazwa na nguvu Zangu na zaidi ya hayo aliyejawa na utukufu Wangu. Hawa aliumbwa kutoka kwa Adamu, kwa hivyo alikuwa pia mfano Wangu, kwa maana yeye alikuwa mtu wa pili kuumbwa kwa mfano Wangu. Maana ya asili ya “Hawa” ilikuwa kiumbe hai, mwenye roho, mwili na mifupa, ushuhuda Wangu wa pili na pia mfano Wangu wa pili miongoni mwa mwanadamu. Walikuwa mababu wa wanadamu, hazina safi na ya thamani ya binadamu, na, kutoka awali, viumbe hai waliojaliwa na roho.

Umetoholewa kutoka katika “Maana ya Kuwa Mtu Halisi” katika Neno Laonekana katika Mwili

Iliyotangulia: 294 Huruma ya Mungu Imemruhusu Mwanadamu Kusalia Hadi Leo

Inayofuata: 296 Huzuni ya Binadamu Aliyepotoka

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki

Wasiliana nasi kupitia WhatsApp