305 Mwenyezi Mungu Wetu Mpendwa

1

Ni nani aliye mkuu na mwenye kuheshimiwa, nani ajaye chini kwa unyenyekevu mahali duni kumwokoa binadamu?

Nani anenaye na mwanadamu, sako kwa bako, ambaye kila neno lake ni ukweli?

Ee, ni Mwenyezi Mungu wetu mpendwa, Mpendwa wetu mkuu!

Unanena na kufanya kazi kati yetu, ukituongoza katika Enzi ya Ufalme.

Unakula nasi, kukaa nasi na unaishi nasi, Uko nasi usiku na mchana.

Maneno Yako huondoa dhana zetu potovu, mioyo yetu inakukaribia.

Unyenyekevu na kujificha Kwako lazima utapendwa sana, tabia Yako ni ya kupendeza na nzuri.

Unawafanya binadamu wasio na maana, wenye kiburi wahisi aibu, pasi na mahali pa kuonyesha nyuso zao.

Kuna mengi ya kupenda kukuhusu, mioyo yetu imejaa upendo na sifa Kwako.

2

Nani atoaye upendo Wake wote kwa binadamu na kuonja mabadiliko ya ulimwengu?

Nani afanyaye bidii usiku na mchana kwa ajili ya binadamu na hutekeleza kazi Yake licha ya shida zote, mwaka baada ya mwaka?

Ee, ni Mwenyezi Mungu wetu mpendwa, Mpendwa wetu mkuu!

Umepitia fedheha, kashfa na kukufuru, uvumi na hukumu nyingi,

lakini tamanio Lako la kuonyesha maneno Yako na kuwaokoa binadamu halijabadilika kamwe.

Umegaagaa na kupinduka usiku mwingi, Usiweze kulala, Ukiwa na wasiwasi kutuhusu na kutujali kila wakati.

Kuacha usingizi na kusahau kula, Unajitoa kabisa kwa ajili yetu na kamwe hujali kuhusu mateso Yako mwenyewe.

Kila hatua ya ukuaji wetu inalipwa kwa damu ya moyo Wako.

Kuna mengi ya kupenda kukuhusu, mioyo yetu imejaa upendo na sifa Kwako.

3

Nani atoaye kila kitu Chake kuwaokoa binadamu kutoka katika nguvu za giza?

Ni nani aonyeshaye mamilioni ya maneno kuhukumu na kumwokoa binadamu?

Ee, ni Mwenyezi Mungu wetu mpendwa, Mpendwa wetu mkuu!

Upo kila wakati, Ukihofia upotovu wetu, Ukihangaikia udhaifu wetu.

Hukumu, ufunuo, kuadibu na ufunzaji nidhamu vyote vinafanywa kututakasa.

Tupitiapo usafishaji na uchungu, upendo Wako uko nasi, maneno Yako yanatufariji na kutuongoza.

Kuhukumiwa, kuadibiwa, kupigwa na kufunzwa nidhamu wakati baada ya wakati hutuwezesha kubadilika.

Kwamba tunaweza kupata utakaso leo ni kwa ajili ya upendo na wokovu Wako.

Kuna mengi ya kupenda kukuhusu, mioyo yetu imejaa upendo na sifa Kwako.

Iliyotangulia: 304 Daima Natamani Sana Upendo wa Mungu

Inayofuata: 306 Niliumbwa na Wewe, Mimi ni Wako

Ulimwengu umezongwa na maangamizi katika siku za mwisho. Je, hili linatupa onyo lipi? Na tunawezaje kulindwa na Mungu katikati ya majanga?
Wasiliana Nasi
Wasiliana nasi kupitia WhatsApp

Maudhui Yanayohusiana

Mipangilio

  • Matini
  • Mada

Rangi imara

Mada

Fonti

Ukubwa wa Fonti

Nafasi ya Mstari

Nafasi ya Mstari

Upana wa ukurasa

Yaliyomo

Tafuta

  • Tafuta Katika Maneno Haya
  • Tafuta Katika Kitabu Hiki